Text

Shika Sana Ulichonacho, Asije Mtu Akaitwaa Taji yako - Sehemu ya I

1 views 1 day ago

Ufunuo 3:11 SUV

“Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.”

MAMBO YA KUJIFUNZA:

1) NAJA UPESI

2) SHIKA SANA

3) ASIJE MTU

NAJA UPESI

Najua sote tunajua umuhimu wa KURUDI KWA YESU, na nini kitatokea Yesu akirudi!!

Yesu atakaporudi ndio mwisho wa wokovu wa Neema!

Yesu atakaporudi ndipo ule mlango alioufungua wa wokovu kwa watu wote utafungwa!

Kwa kujua UMUHIMU WA KURUDI KWAKE, Yesu anatufikishia ujumbe huu kwamba NAJA UPESI, akiambatanisha na maelekezo mawili muhimu sana ili KUJA KWAKE KUWE NA MAANA KWAKO!

SHIKA SANA ULICHO NACHO

1) Maana yake ulicho nacho kinashikika

Ulicho nacho, ni wokovu ulioupokea kwa Yesu! Kama una wokovu utajua tu; kama maisha yako yako salama utajua tu!

Wokovu ni halisi! "Unashikika"

2) Maana yake, usipokuwa makini unaweza ukakiachia au kukipoteza

Usipoujali wokovu unaweza ukaupoteza!

“sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii?" Waebrania 2:3 SUV

Ukiona hujali tena mambo ya Mungu, ujue unaelekea kuupoteza wokovu

Na ukiupoteza maana yake sio rahisi kupona au kuiponya nafsi yako!

3) Maana yake kama unacho utajua tu unacho

- Kwa hiyo kama huna uhakika na wokovu wako, una wezekano mkubwa kwamba ulishaupoteza; aliye na kitu cha thamani anafahamu kuwa anacho

4) Maana yake, wewe ndio unao wajibu wa kushika sio mwingine!

Kuna watu wanavuruga maisha ya wokovu na hawataki kubeba wajibu na kujirekebisha... Wanabaki kujitetea, yaani mimi niliokoka kabisa ila mazingira ninayoishi au wazazi au ndugu, wengine husema wachungaji wao ndio wamesababisha nk!

Ukitaka kufanikiwa katika wokovu, kubali kuwajibika na yale usiyofanya sawa sawa na wokovu!

ASIJE MTU

- Kitu hatari kuliko yote kwenye kuharibu wokovu wa mtu, ni MTU!

- Ndio maana Yesu akasema ASIJE MTU...

- Sasa hatuishi na MTU kama KITU! Tunaishi na mtu au watu kwa mahusiano!

KIMSINGI ALICHOKUWA ANASEMA YESU NI KWAMBA, TUWE WAANGALIFU TUNAVYOHUSIANA NA WATU!

Hajasema asije Shetani akaitwaa taji yako, amesema "asije mtu akaitwaa taji yako"‼ANZA KUFUATILIA KUANZIA UMEANZA KUHUSIANA NA HUYO MTU, TAJI YAKO IMESHAMEGWA KIASI GANI?

Ni kwa kiasi gani umeshapoteza utukufu wa Mungu maishani mwako tangu HUYO MTU aingie kwenye maisha yako?

Ni kiasi gani umekuwa mkame tangu huyo mtu ameingia kwenye ratiba zako...

Karibu kila mtu ukifuatilia chanzo cha anguko lake utagundua wengi au wote kilianzia alipokutana na mtu fulani!

Shetani hawezi kuja na mapembe, atatumia mtu uliyemzoea.

“Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.” UFU. 3:11 SUV

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!