Siku Zote Amua Kuwa Upande wa Mungu
2 Samweli 24:14
“Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na tuanguke katika mkono wa BWANA; kwa kuwa rehema zake ni nyingi; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu.”
Daudi alipomkosea Mungu, nabii Gadi alitumwa na Mungu kumletea adhabu tatu achague mojawapo kati ya hizo.
2 Samweli 24:12 “Nenda, ukanene na Daudi, BWANA asema hivi, Nakuwekea mambo matatu; katika haya uchague moja, nikutendee hilo.”
Adhabu zenyewe zilikuwa zifuatazo:-
1. Miaka saba ya njaa
2. Miezi mitatu ya kukimbia mbele ya adui zake
3. Siku tatu za tauni nchi nzima
Baada ya kujitafakari Daudi akaona haelewi, ni kama vile adhabu zote ni kubwa mno kwake, Daudi akaamua kuwa upande wa Mungu ndipo akajibu "basi sasa na tuanguke katika mkono wa BWANA"
Ninaamini kuna jambo kubwa sana la kujifunza hapa.
Kuna wakati katika maisha unaweza ukafika mahali ni kama vile pande zote umebanwa, wakati mwingine huoni mahali pa kupumulia..
Katika hali hizo mara nyingi Shetani atakuambia umlalamikie na kumnung'unikia Mungu..
Shetani atataka uone kama Mungu anakutesa na hakupendi..
SIKU ZOTE CHAGUA UPANDE WA MUNGU.
HATA KAMA HUMUELEWI MUNGU NA HAUELEWI UNACHOKIPITIA.
HATA KAMA UNAONA KAMA MBINGU ZIMEKAA KIMYA, HAUSIKII SAUTI YA MUNGU KUHUSIANA NA JAMBO HILO.
Ni kama options zote ulizo nazo ni mbaya hakuna unafuu upande wowote..
CHAGUA KUANGUKIA UPANDE WA MUNGU... CHAGUA KUAMINI MUNGU NI MWEMA NA ANAKUWAZIA MEMA... CHAGUA KUAMINI KWAMBA MUNGU HAJAKUACHA NA ATAKUVUSHA.
CHAGUA KUAMINI UPENDO WA MUNGU USIOKOMA HATA WAKATI WA CHANGAMOTO NA MATESO.
Ayubu 19:25 “Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai,
Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.”
2 Wakorintho 4:8-9 “Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa; twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi;”
Chagua kuangukia mikononi mwa Mungu hata wakati unaona dhiki kila upande, shaka kila upande, maudhi kila upande...
Unaweza usiweze kuzuia dhiki, LAKINI UNAWEZA KUZUIA MOYO WAKO USISONGWE, unaweza kushindwa kuzuia hali za mashaka lakini, UNAWEZA KUZUIA USIKATE TAMAA.
Daudi alikuwa anajua wazi kwamba, kinachomkabili ni matokeo ya dhambi yake lakini bado hakumkimbia Mungu, aliamua kuangukia upande wa Mungu, Mikononi mwa Mungu.
Hata tukikosea bado MAHALI PETU SALAMA NI MIKONONI MWA MUNGU.
Usikubali Shetani akakutenga na Mungu kwa kumlaumu au kumnung'unikia eti kwa sababu ya changamoto unayopitia..
Hakikisha Shetani mwenyewe anajua kwamba WEWE NA MUNGU WAKO HAMUWEZI KUKOSANA HATA KAMA HAJAJIBU KAMA ULIVYOTARAJIA.
Kisiwepo cha KUKUTENGA NA UPENDO WA MUNGU
Warumi 8:37-39 “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
Ukifuatilia maandiko katika 2 Samweli 24 utagundua Mungu alichagulia Daudi adhabu ya Tauni ya siku tatu, lakini ile tauni ilikaa siku moja tu na Mungu mwenyewe akamzuia malaika aliyeileta na kisha AKAMUELEKEZA DAUDI NINI CHA KUFANYA ILI TAUNI IKOME KABISA.
2 Samweli 24:15-16,18-19,25 “Basi BWANA akawaletea Israeli tauni tangu asubuhi hata wakati ulioamriwa; nao wakafa watu toka Dani mpaka Beer-sheba sabini elfu. Lakini huyo malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili auharibu, BWANA akaghairi katika mabaya, akamwambia huyo malaika mwenye kuwaharibu watu, Yatosha, sasa ulegeze mkono wako. Naye yule malaika wa BWANA alikuwako karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi. Siku hiyo Gadi akamwendea Daudi, akamwambia, Haya! Kwea wewe, ukamwinulie BWANA madhabahu penye kiwanja cha Arauna, Myebusi. Basi Daudi akakwea sawasawa na neno la Gadi, kama BWANA alivyoamuru. Naye Daudi akamjengea BWANA madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Basi BWANA aliiridhia nchi, na tauni ikazuiliwa katika Israeli.”
Siku zote Mungu anatuwazia mema hata kama HATUELEWI KINACHOENDELEA. TUNAPASWA KUCHAGUA UPANDE WA MUNGU NA KUENDELEA KUMTAFUTA MPAKA TULIDAKE WAZO LAKE NA MAELEKEZO YAKE YA KUTUVUSHA TULIPOKWAMA.
Yeremia 29:11 “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.”
Jiambie mwenyewe ukimaanisha:-
"NINAJUA MUNGU ANANIWAZIA MEMA NA ATANIVUSHA HATA KAMA SIELEWI. HATA KAMA NAONA KIMYA, NINAJUA MTETEAJI WANGU YU HAI NA SIKU MOJA ATASIMAMA JUU YA NCHI. NIMECHAGUA KUANGUKIA MIKONONI MWA MUNGU HATA KAMA SIELEWI"
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
#Umebarikiwa
~Na Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author