Text

Siri ya Furaha ya Kudumu

1 views 1 day ago

Wafilipi 4:4

"Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini."

Agizo hili la kufurahi katika Bwana siku zote maana yake ni kwamba; "siku zote, chanzo cha furaha yangu na yako kinapaswa kuwa ni BWANA YESU"!

Kuna maneno matatu napenda kuyaelezea kwa undani kidogo katika msitari huo:-

1. FURAHINI,

2. KATIKA,

3. BWANA

Neno la kwanza lina maana ya KUJIFURAHISHA, au KUFURAHIA

Neno la pili lina maana KWA SABABU YA, au NDANI YA, KATIKA UWEPO WA, au HUKU UKIMFIKIRIA

Na Neno la tatu (Bwana) lina maana MMILIKI HALALI, ANAYEWAMILIKI, MWENYE UWEZO WA KUMUAMULIA MTU!

Sasa turudi kwenye andiko letu la kutafakari:-

"Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini."

Likiwa na maana kuwa, TUNAPASWA KUJIFURAHISHA AU KUFURAHIA KWA SABABU YA, au KATIKA UWEPO WA au HUKU TUKIMFIKIRIA BWANA YESU (Ambaye ndiye mmiliki wetu na mwenye uwezo wa kuamua kila kitu kutuhusu sisi)!

Kwa hiyo, KABLA YA KUFURAHI, LAZIMA UHUSIANE NA YESU KAMA BWANA KWAKO! Kama mmiliki wako, kama mfalme wa amani yako, kama yeye ndiye chanzo cha furaha yako!

Ni lazima YESU AWE NI BWANA WAKO KWELI NA SIO MDOMONI TU, ndipo ataweza kuwa chanzo cha furaha yako!

Kumbe KILE UNACHOKIRUHUSU KUWA CHANZO CHA FURAHA YAKO HICHO NDIO BWANA WAKO, MAANA UNAJIFURAHISHA KWACHO!

Yesu akiwa BWANA KWAKO atakuwa ndio CHANZO CHA FURAHA YAKO, kwa hiyo utaweza "KUFURAHI KATIKA BWANA SIKU ZOTE"

Kufurahi katika Bwana maana yake, UNAFURAHI KWA SABABU YA BWANA YESU AMBAYE HABADILIKI SIKU ZOTE!

Sifurahi kwa sababu nina pesa au kwa sababu mambo yangu yote yanaenda vizuri bali nafurahi kwa sababu NINAYE BWANA ASIYEBADILIKA NA ANAWEZA KUGEUZA CHOCHOTE HATA KAMA HAKIENDI VIZURI!

Kama FURAHA YANGU INATEGEMEA PESA/MALI YANGU MAANA YAKE PESA/MALI NDIO BWANA WANGU maana SIKUZOTE furaha ina connection na Bwana!

Imarisha uhusiani wako na YESU KAMA BWANA, utajikuta Yeye NDIO CHANZO CHA FURAHA YAKO SIKU ZOTE!!

-- Tafakari ya leo inatukumbusha, FURAHA YETU SIKU ZOTE IWE KWENYE MSINGI WA UHUSIANO WETU NA YESU KAMA BWANA WETU, na sio kwenye VITU VINAVYOONEKANA maana vinavyoonekana vyote si vya kudumu!!

-- Kuna watu wanakosea na kuwaambia watu wao wakaribu, watoto wao au wapenzi wao kwamba "WEWE NDIO FURAHA YANGU!" Ni kweli tunahitaji kuwafurahia watu lakini HAKUNA MTU ANAFAA KUPEWA KAZI HII YA KUWA CHANZO CHA FURAHA, hiyo ni kazi ngumu mno, NI YESU TU NDIO HATAKUANGUSHA UKIMFANYA CHANZO CHA FURAHA YAKO!!! Wengine wote watafika mahali watakuangusha...

Hata kama wasipokuangusha (ku-let down) Ni vizuri pia kufahamu kila binadamu atakufa, kwa hiyo sio sahihi kumfanya kuwa yeye ndio chanzo cha furaha yako!

--Ukitaka KUFURAHI SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO bila kujali nini kinaendelea huku duniani, BASI MFANYE YESU CHANZO NA SABABU YA FURAHA YAKO!

“Nawe utajifurahisha kwa BWANA, Naye atakupa haja za moyo wako.”

Zaburi 37:4 SUV

KUNA HAJA ZA MIOYO YETU ZINGINE ZIMEFUNGWA KATIKA KUJIFURAHISHA KWA BWANA, ukifurahi kwake tu anaziachilia!

"Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini." 

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!