Sisi Hatumo Miongoni Mwao Wasitao na Kupatwa na Uharibifu
Waebrania 10:39
“Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.”
Hebrews 10:39 ISV
“Now, we do not belong to those who turn back and are destroyed, but to those who have faith and are saved.”
Neno hilo nililonukuu lina mambo muhimu sana ambayo nimeona ndani yangu wana wa Mungu tujikumbushe.
Neno hilo "Sisi" naweza kusema ni neno la "kibaguzi".
Neno "Sisi" linapotumika linamaana kuna "Wao" ambao ni tofauti na "sisi".
Ukiendelea na maneno yanayofuata utagundua anaongelea hapo kuna makundi mawili... Sisi na wao.
Na anaelezea hilo kundi la pili (la wao) sifa zao kubwa ni KUSITA na KUPOTEA.
Ni kundi la watu wanaosita sita na kupotea.
Ukisoma mstari mmoja kabla (wa 38) utaona kitu kinachoungana (connect) na hiki cha mstari huu wa 39.
Waebrania 10:38-39 “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.”
Mstari wa 38 unaonyesha kuwa, kundi hili la pili (la wao), laweza kuwa ni wenye haki (yaani wameokoka) lakini hawaishi kwa IMANI bali wamejaa kusitasita, wasiwasi na mashaka...
Lakini pia inawezekana ni mtu asiye mwenye haki wa Mungu kabisa (yaani, mtu ambaye hajampa Yesu maisha yake) hana imani ya kweli na amejaa mashaka na kusitasita.
Hawa wote wawili wanawekwa kundi moja la watu ambao Mungu hana furaha nao.
Sasa tukumbuke, Haki ya Mungu inapatikana kwa Imani katika Kristo Yesu, kwa hiyo tunapopoteza imani, haki yetu katika Kristo inakuwa mashakani. Yaanihatutafurahia haki yetu katika Kristo.
Na Neno linasema Mungu hana furaha na hao watu...
Lakini pia, Neno linasema FURAHA YA MUNGU ndio nguvu zetu...
Kwa hiyo ni wazi, MTU WA KUSITASITA (Asiye na Imani) NI MTU ASIYE NA NGUVU ZA MUNGU (NI MTU DHAIFU), au ni mtu ambaye ni rahisi KUSHAMBULIWA NA UDHAIFU ikiwemo MAGONJWA mbalimbali.
Maisha ya IMANI NI MAISHA YA ULINZI, MAISHA YA KUSITASITA NA MASHAKA NI MAISHA DHAIFU.
Sasa turudi kwenye andiko letu kuanzia pale tulipoishia.
Waebrania 10:39 “Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.”
Kwa hiyo, kuna kundi la wao (wasitao na kupotea) na kuna sisi (tulio na imani ya kutuokoa).
Neno linasema sisi SIO SEHEMU YA WAO.
Sisi hatumo MIONGONI MWAO.
Nataka niingie ndani kidogo kwenye maneno yaliyotumika hapo ili iwe rahisi kueleweka.
Hayo maneno ni "WASITAO NA KUPOTEA"
Kusita na kupotea - Ni hali ya kurudi nyuma kunakosababishwa na Hofu ya kinachokukabili au kinachowakabili na matokeo yake ni kupata uharibifu... Au kupatwa na unachokiogopa.
Hilo Neno "KUPOTEA" NI KUPATA MADHARA... Sasa haya ni madhara ya kile unachokiogopa au kile kilichosababisha hali ya KUSITA SITA (HOFU, WOGA, WASIWASI NA KURUDI NYUMA).
Kuna watu wamerudi nyuma SABABU YA HOFU...
Kuna watu wameacha kwenda KANISANI SABABU YA HOFU...
Neno la Mungu linasema, watu hao WATAPOTEA AU WATAPATA UHARIBIFU...
Sasa, SISI HATUMO MIONGONI MWA HAO WASITAO... WALIO NA HOFU NA MASHAKA...
SISI AMBAO HATUMO MIONGONI MWAO TUNA SIFA ZETU...
"bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu."
Sisi tumo katika kundi la WENYE IMANI IOKOAYO...
Sisi tuna imani za kutuokoa... Imani zetu sio bure bali ZINA WOKOVU NDANI YAKE...
Imani yetu inaweza kutuokoa na kila uangamivu wote wa shetani na mapepo yake na magonjwa yake yote, na hata tauni iharibuyo.
Zaburi 68:20 “Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa;”
Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana.
Mungu kwao anaweza kuwa na mipaka katika kuokoa na kuwatoa mautini, LAKINI SIO KWETU SISI... KWETU SISI NI MUNGU WA KUOKOA NA KUTUTOA MAUTINI...
Kinachomfanya kwao asiwe wa kuokoa sio kwamba Mungu anabadilika, lakini ni kwa sababu wao hawamuamini kama NI MUNGU WA KUOKOA... NI KWA SABABU WAMEJAA MASHAKA, HOFU NA KUSITASITA.
Kuanzia sasa ujiambie, "MIMI SIMO MIONGONI MWAO WASITAO NA KUPOTEA BALI NINAYO IMANI INAYOWEZA KUNIOKOA NA KILA AINA YA UHARIBIFU."
Jiambie, "Mungu wangu ni Mungu wa kuokoa, na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana"
Kama ulikuwa miongoni mwao wasitao, FANYA MAAMUZI LEO YA KUHAMA KUNDI, TOKA KWENYE KUNDI LA WASITAO, WENYE HOFU NA WASIWASI NA WANAOPOTEA, INGIA UPANDE WA USHINDI.
Kama ulikuwa hujampa Yesu maisha, ni bora kufanya hivyo (kuokoka) sasa. Na kama ulikuwa umeokoka lakini umekaa kundi la wao kwa sababu ya wasiwasi, hofu na kusitasita, fanya maamuzi haraka kutoka huko.
Na kama umeamua kutoka UPANDE WA WASITAO NA HOFU, hakikisha UNAACHA PIA KUFUATILIA HABARI ZA KUNDI LA WASITAO.
Acha kufuatilia habari za HOFU, WASIWASI NA KUSITASITA.
Anza kufuatilia HABARI ZA KUNDI LAKO... HAKIKISHA UMEJAA HABARI ZA IMANI INAYOOKOA KULIKO HABARI ZA HOFU.
Habari za Imani ni Neno la Mungu, kwa sababu IMANI HUJA KWA KUSIKIA NENO LA KRISTO.
JITOE KWA WASITAO, JITOE KWA KUNDI HILO BAYA SABABU LINAISHIA KUPOTEA.
Waebrania 10: 38 “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani;”
IMANI NDIO HUTUPATIA MAISHA SISI WA KUNDI HILI...
HUWEZI KUISHI KUNDI HILI KAMA HUNA IMANI... IMANI NDIO HUTUPA MAISHA, NDIO HUTUPA UHAI NA UZIMA...
UHAI NA UZIMA WETU HAUKO KWENYE VITU, UKO KWA KRISTO KWA NJIA YA IMANI.
Piga kelele sema "MIMI SIMO MIONGONI MWAO WASITAO NA KUPATA UHARIBIFU"
1 Yohana 5:4 “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.”
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author