Sisi (Mimi) Sio Kama Wao
ISA. 57:19
“Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya.”
Unataka Amani? Angalia midomo yako inasema nini.
Unataka uponyaji? Angalia midomo yako inasema nini.
Mungu anayaumba matunda ya midomo yetu!
Neno la Mungu linasema “Msiseme, Ni fitina, katika habari za mambo yote ambayo watu hawa watasema, Ni fitina; msihofu kwa hofu yao, wala msiogope.”
ISA. 8:12 SUV
Sisi ni tofauti na wao, sio lazima kinachowapata walio nje ya Yesu kitupate na sisi!
Sisi ni wa ufalme mwingine!
Hatuwezi kusema ni "fitina" kwa jambo ambalo dunia inasema ni "fitina", hatuwezi kuhofu kwa hofu zao.
Kinachowaogopesha wao hakituogopeshi sisi! Maana sisi sio kama wao
Sisi ni uzao mwingine, Sisi si wa mbegu iharibikayo bali wa mbegu isiyoharibika!
“Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.”
1 PET. 1:23 SUV
Sisi hatupatwi na uharibifu wa dunia, sisi hatufungwi na uchumi wa dunia au wa nchi tunayoishi... Sisi tuna mfumo mwingine wa kiuchumi... Sisi ni wa upande mwingine
Sisi tumejiungamanisha na kanuni za uchumi wa ufalme wa Mungu!
Sisi hatufungwi na kanuni za kufanikiwa za kidunia, kanuni zetu ni tofauti na hazizuiliwi na mfumo wa dunia...
Sio lazima wanapolia njaa na sisi tulie njaa, sio lazima wanapolia ajira na sisi tulie ajira, sio lazima wanapolia vyuma vimekaza na sisi tulie kilio hicho hicho...
Sisi sio kama wao.
"OUR CASE IS DIFFERENT"
Ugonjwa unaoitia hofu dunia sisi haututii hofu! KWA SABABU KWENYE UFALME WA MUNGU HAKUNA KITU KINAITWA UGONJWA USIOPONA!
Hatuwezi kuhofu kwa hofu yao hata kama tukikutana na changamoto ile ile inayowapata wao kwa sababu:-
- Sisi tunaye tabibu mkuu (the great physician) anayetibu kila ugonjwa kwa hiyo hatuwezi kuhofu magonjwa kwa hofu zao
- Mungu wetu ndio mtoa riz iki (God our provider) - Jehova Jire; kwa hiyo hatuwezi kuhofu maisha kwa hofu zao maana chanzo cha kipato chetu ni Mungu sio watu wala mfumo!
- Sisi tunaye aliyetoa kodi ya kaisari ndani ya tumbo la samaki, kwa hiyo hatuwezi kuhofu kodi za serikari na bei ya vitu kupanda kama wao!
- Sisi tunaye mtuliza dhoruba, dhoruba haitutishi! Ikichafuka ataituliza...
- Sisi tunaye Bwana wa Vita, kwa hiyo Vita za kibinadamu, kichawi, kiroho, maofisini, kwenye huduma nk haitutishi!
- Sisi tunaye mtetezi aliye hai, na hakimu wa kweli kwa hiyo wanaojaribu kutuonea hawatutishi!
- Sisi tunaye anayeweza kuifanya mikate mitano na samaki wawili kula watu zaidi ya elf 5, kwa hiyo upungufu haututishi!
USISEME NI FITNA WANAPOSEMA NI FITNA, USIHOFU KWA HOFU ZA WANAOKUZUNGUKA MAANA WEWE SIO KAMA WAO, WEWE NI NAMBA NYINGINE!
YOU HAVE A SUPERNATURAL GOD so you are a supernatural creature too! - Tunaye Mungu asiye wa asili ya dunia hii, kwa hiyo na sisi ni viumbe wasio na asili ya kidunia....
Amini na kukiri kile NENO LA MUNGU LINASEMA MAISHANI MWAKO, maana Mungu anayaumba matunda ya midomo yako naye ATAKUPONYA NA KUKUVUSHA!
“Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.”
ZAB. 46:2-3 SUV
Yaani Shetani hata UTETEMESHE NCHI NA MILIMA, HATA MAJI YAVUME NA KUUMUKA HATUOGOPI...
Yaani hata uibuke ugonjwa wa kuangusha kila aliyetuzunguka na aliye karibu nasi, kwa mujibu wa Neno la Mungu, huo ugonjwa bado uko mbali nasi, maana SISI SIO KAMA WAO!
LAZIMA UJITOFAUTISHE NA DUNIA INAYOKUZUNGUKA, KWA SABABU WEWE SIO KAMA WAO...
USIFANYE HUKUMU AU MAAMUZI KWA KILE UNAONA KINAIPATA DUNIA AU UNACHOONA WATU WANASEMA, WEWE SIO WA DUNIA!
WEWE NI MBARIKIWA, WEWE UNAYE MUNGU!
INUKA UAGAZE, ACHA KUJIKUNYATA...
MISRI NA ISRAEL NI TOFAUTI...
Jitangazie mwenyewe, "Mimi sio kama wao , siwezi kufa kifo chao, siwezi kuangushwa na kilichowaangusha, siwezi kutishwa na kinachowatia hofu duniani..."
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
Mwl. Francis Langula
Author