Text

Siyo Mimi Ninayeishi Bali Kristo Yu Hai Ndani yangu

1 views 1 day ago

Wagalatia 2:20 SUV

“Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.”

MAMBO YA KUJIFUNZA:

Kila aliyeokoka hili jambo limefanyika kwake, amesulubiwa pamoja na Kristo, kwa hiyo si yeye tena anyeishi bali Kristo ndio anaishi ndani yake!

Mpaka tutakapoanza kujiona hivyo, kujifikiri hivyo na kujitambua hivyo ndipo tutaanza kumdhihitisha Yesu kwa maisha yetu

Kama nimesulubiwa pamoja na Kristo maana yake sina maisha yangu binafsi, MAISHA NINAYOISHI NI MAISHA YA YESU NDANI YANGU, ya kwangu yalishasulubiwa!

Sio mimi ninayeishi bali Yesu ndani yangu, yaani mimi na Yesu tu mmoja!

Shetani hawezi kunipata maana address yangu ilishapotea duniani, nilishaisulibiaha akinitafuta anakutana na Yesu!

Magonjwa pia hayaelewi nilipo maana yakinitafuta yanamkuta Yesu!

Kama maisha yangu yalisulibishwa pamoja na Kristo halafu sio mimi ninayeishi tena bali Kristo ndani yangu basi SINA MAISHA AINA MBILI TENA, eti maisha yangu ya kawaida na maisha yangu ya wokovu! Maisha yangu ni aina moja tu YESU NDANI YANGU!

Sina maisha ya aina mbili tena kwamba, MAISHA YA WOKOVU nikishindwa MAISHA YA DUNIA! Sina choices tena! 

Maadamu ninaishi mimi ni kwa ajili ya YESU, zaidi ya hapo NIMEKUFA!

Ndio maana Paulo alisema "KUISHI NI KRISTO" kwake yeye KUISHI MAANA YAKE NI KRISTO ANAISHI baada ya hapo ni KUFA!

Kama KRISTO anaishi ndani yangu, na maisha yangu yalisulibishwa basi KUKATA TAMAA NA KURUDI DHAMBINI SIO OPTION TENA KWANGU!

Kujibiwa maombi yangu au kutojibiwa sio kigezo cha kuendelea na wokovu au la; kwa sababu sina upande wa pili, nina upande mmoja tu KRISTO NDANI YANGU!

Hili Neno linakuwa halisi kwangu kwamba “Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai.” Matendo ya Mitume 17:28 SUV

Yaani NJE YA MUNGU I AM DEAD! 

BINAFSI SIJIONI NIKIISHI NJE YA YESU

ILI NIISHI NI LAZIMA IWE TU NDANI YAKE YEYE, NDANI YA KRISTO!

“Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.” Wakolosai 3:3 SUV

Maisha ya aina hii yanaku guarantee ulinzi wa Mungu 100% 

KILA ALIYEOKOKA ANAPASWA KUJIONA HIVYO KWA SABABU NDIVYO ALIVYO!

Pamoja kwamba ndivyo tulivyo, lakini Mungu hawezi kujidhihirisha kwako zaidi ya UNAVYOJIONA NA UNAVYOMUONA MUNGU KWAKO!

Acha kujitenganisha na YESU, YUKO NDANI YAKO KWA NJIA YA ROHO WAKE! Ukiomba hatokei Mbinguni kukujibu, anajidhihirisha toka ndani yako!

Ukiombea Mgonjwa, nguvu haitokei mbinguni kumponya mgonjwa, inatoka ndani yako kumponya mgonjwa!

Kama unaumwa na una Roho Mtakatifu ndani yako, nguvu ya kukuponya haitoki mbinguni, inatoka humo humo ndani yako! Na ni nguvu hiyo hiyo ukiiruhusu inaweza kutunza afya yako mbali na magonjwa!

Kama unaumwa, unaweza ukaamua kutafakari kipande hiki cha andiko "wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu;" ukikitafakari kwa mida wa kutosha nankukielewa, inuka ujicheki utagundua umeshapona!

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!