Text

Songa Mbele

1 views 1 day ago

Wafilipi 3:13-14

“Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.”

Kuna vitu viwili vinaweza kutukwamisha kufikia UKUU ambao Mungu ametukusudia maishani mwetu.

Moja ni MAFANIKIO MADOGO na pili ni KUKOSEA AU KUSHINDWA.

Haya yote mawili yamewahi kuwakwamisha watu wasifikie hatma zao.

Kuna watu baada ya kufanikiwa MAFANIKIO MADOGO, nayaita mafanikio madogo kwa sababu, hata kama yalionekana makubwa bado hayakuwa kwa kiwango ambacho Mungu alitaka kumfikiksha huyo mtu kama asingekwamia hapo; Yaani watu hao walipofanikiwa kidogo wakabaki wanayatazama mafanikio hayo na kuacha KUTAZAMA HATMA KUBWA AMBAYO MUNGU AMEWAANDALIA MBELE, wakadhani wamefika

Kabla hujafa, hata kama unafikiri umefanikiwa kwa kiwango gani, BADO HUJAFIKIA MWISHO WA KUFANIKIWA.

Kuna watu kilichowamaliza ni pale alipopata pesa kiasi fulani na akahisi amefanikiwa, wengine walipopata kiwango fulani cha elimu akahisi amefika na ndio ilikuwa anguko lake, wengine alipojenga, aliponunua gari, alipopata kazi fulani, mwingine alipoweza kuhubiri, kuponya, kutoa pepo, kuwa na kanisa nk.

Ukweli ni kwamba, mafanikio ya Ki-Mungu hayana mwisho, maadamu bado tunaishi, hatuwezi kufikia mwisho, bado kuna hatua nyingine mbele yetu kwa hiyo si sawa kukwamia kwenye mafanikio aina yoyote.

Sifa mojawapo ya MAFANIKIO YA KI-MUNGU, ni MAFANIKIO YASIYOKOMA, kwa sababu MUNGU HANA UKOMO, NI MAFANIKIO YASIYO NA MWISHO SABABU MUNGU HANA MWISHO.

Neno la Mungu linasema katika Mithali 4:18 "Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo, Ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu."

Tunapaswa kuendelea kung'aa mpaka mchana mkamilifu.

Mungu wakati anapanda mbegu ya mafanikio ndani ya Adam alimwambia hivi

Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”

Jambo ambalo kwa namna yoyote ile Adam na Eva wasingeweza kulikamilisha peke yao, ni wazi kwamba walikuwa wazae, waongezeke, wawaachie kijiti wengine waendeleleze kuzaa na kuongezeka.

Kwa lugha nyingine, kuzaa na kuongezeka ni kufanikiwa kwa kile tunachokifanya. Biashara ikizaa na kuongezeka imefanikiwa, huduma vile vile, lakini haijafikia mwisho. Huwezi kuyamaliza mafanikio aliokupangia Mungu, utafanikiwa na kufanikiwa kisha utawaachia wengine waendelee kufanikiwa.

Usikubali mafanikio yakukwamishe, usikubali kujiona umefika mwisho, tunapaswa kuyachukulia mafanikio kama hatua au ngazi ya kutupeleka ngazi nyingine.

Lakini pia kwa upande wa pili, KUSHINDWA au KUKOSEA kumewakwamisha wengi.

Kimsingi kinachokwamisha sio KUKOSEA bali ni UNAFANYA NINI BAADA YA KUKOSEA.

Ninajua MAKOSA YANAPISHANA lakini UKWELI NI KWAMBA, MAADAM TUNAISHI DUNIANI, TUKIFANYA MAAMUZI SAHIHI TUNAWEZA KUTOKA KATIKA KILA KOSA AU KUSHINDWA NA KUENDELEA MBELE.

Wengi waliokwama sababu ya makosa, WALICHUKULIA MAKOSA KAMA SHIMO WASILOWEZA KUTOKA.

Kama vile mafanikio yasivyotakiwa kutukwamisha kwa maelezo niliyoweka hapo juu, ndivyo ambavyo MAKOSA AU KUSHINDWA hakupaswi kutukwamisha.

Maandiko niliyonukuu hapo mwanzo kabisa wa tafakari hii yameweka vizuri sana kitu ninachokieleza hapa.

Neno linasema "Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.

Wakati Paulo anaandika waraka huu, alikuwa tayari ni Mtume aliyefanikiwa sana ukilinganisha na mitume wengine wote.

Alikuwa ameshafungua makanisa mengi na hii ni moja ya nyaraka zake kwa makanisa yake.

Kimsingi hapa Paulo anasema, PAMOJA NA KWAMBA NIMEFANIKIWA, "sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika"

Yaani ndani ya moyo wangu sijioni nimekwisha KUSHIKA KILE MUNGU AMEKUSUDIA MAISHANI MWANGU. Ndani yangu sijioni nimefika mwisho wa mafanikio aliyonikusudia Mungu.

Kisha anasema, ninang'ang'ana na Neno moja tu, "nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele".

Yaani, siruhusu mafanikio yangu ya sasa yanizuie kufanya kitu au vitu sahihi ili niendelee kupiga hatua zaidi kuelekea kiwango cha mafanikio Mungu aliyonikusudia.

Lakini, YALIYO NYUMA SIO MAFANIKIO TU BALI HATA MAKOSA NA KUSHINDWA, kwa hiyo anasema SIRUHUSU MAKOSA YANGU YANIZUIE KUYACHUCHUMILIA YALIYO MBELE YANGU.

Anamalizia na kusema "nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu"*

Kuna mambo matukufu mbele yetu yanayopaswa kutufanya tusikwamishwe na mafanikio wala makosa yetu.

Kama unafikiri umefanikiwa, basi HUJAONA KIWANGO CHA MAFANIKIO YALIYO MBELE YAKO, UKIONA HUTAISHIA HAPO UTASONGA MBELE.

Na kama unafikiri UMEKOSEA AU UMESHINDWA HUJAJUA MPANGO MZURI MUNGU ALIYOWEKA MBELE YAKO IKIWA UTAAMUA KUREKEBISHA NA KUSONGA MBELE.

Ukifanya jambo zuri leo, litie kapuni endelea KUKAZA MWENDO, usidhani umefika na kulibeba hilo miaka... KUNA MEDE YA THAWABU INAKUNGOJA MBELE... Vilevile UKIKOSEA usikwamie hapo, rekebisha haraka SONGA MBELE.

KATIKA HALI YOYOTE ULIYOPO SASA, SONGA MBELE, KUNA MEDE YA THAWABU MBELE YAKO INAKUNGOJA.

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!