Tumaini Kwa Mungu, Kutulinda na Madhara ya Miili Yetu
Danieli 6:23
Ndipo Danieli akatolewa katika lile tundu, wala halikuonekana dhara lolote mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake.
Kuna kitu nimekiona kwenye andiko hilo, na ningependa tukione pamoja.
Kilichosababisha madhara yasiupate mwili wa Daniel ni KUMTUMAINI MUNGU.
Ninaamini hii ni kanuni ambayo inaweza kumsaidia kila mtu, hata mimi.
Nikimtumaini Mungu, madhara hayawezi kuupata mwili wangu.
Kama SIMBA hawakuweza kuudhuru mwili wa Daniel, vipi kuhusu vijidudu vya magonjwa mbali mbali?
Ninaamini kwa mtu anayemtumaini Mungu, hata akiletewa virusi vya HIV na mkewe au mumewe, HAVIWEZI KUUDHURU MWILI WAKE.
Hata nikiwa mwenye mazingira hatarishi, tumaini langu kwa Mungu linaweza kunilinda na madhara.
So Daniel was taken out of the den, and no injury whatever was found on him, because he believed in and relied on and trusted in his God. DANIEL 6:23 AMP
Hilo Neno KUMTUMAINI MUNGU lina maana, KUMUAMINI (Believing), KUMTEGEMEA (Relying on) NA KUMTUMAINIA (Trusting in) Mungu.
Kwa hiyo si tu kutumaini kama inavyochukuliwa kirahisi rahisi.
Kwa hiyo, ninaweza kumtumaini Mungu kunilinda na madhara yoyote ya mwili wangu, hata kama mahali ninapofanyia kazi hakuna usalama wa kutosha.
Daniel alikuwa kwenye mazingira hatarishi kabisa kwa usalama wa Mwili wake, lakini TUMAINI LAKE KWA MUNGU LILIULINDA MWILI WAKE DHIDI YA SIMBA.
KUTODHURIKA KWA MWILI WANGU HAKUTEGEMEI usalama wa mahali nilipo bali KUNATEGEMEA TUMAINI LANGU KWA MUNGU.
Sasa hii haimaanishi tusijali usalama wa mazingira yetu, lakini kuna wakati swala la USALAMA WA MAZINGIRA YETU linakuwa nje ya uwezo wetu kama vile Daniel.
Kwa mfano, mtu anafanya kazi mgodini na analazimika kupigwa na vumbi la migodini, au mtu anafanya kazi kiwanda fulani na kuna madhara ya kiafya yanayoweza kusababishwa, MTU HUYU ANAWEZA KABISA KUAMUA KUMTUMANI MUNGU, NA YALE MAZINGIRA YASISABABISHE MADHARA KABISA.
Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Mithali 3:5
Hata kwa eneo la afya za miili yetu, tumtumaini Mungu, na tusizitegemee akili zetu.
Akili zinapaswa kutumiwa tu na si kutegemewa.
Ndio maana Neno linasema "wala hakuna chochote kitakachowadhuru" Luka 10”19
Tukiijua hii haki yetu, tutagundua sisi tuna asili ya KUTODHURIKA NA CHOCHOTE, MAGONJWA NA KILA SHAMBULIO LA ADUI haviwezi kutudhuru.
Hiyo ni haki yako, USIKUBALI CHOCHOTE KUUDHURU MWILI WAKO, WEWE NI KIZAZI KISICHODHURIKA.
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
Mwl. Francis Langula
Author