Text

Tusichoke Kutenda Mema

1 views 1 day ago

Isaya 3:10

“Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao”

Wagalatia 6:7,9-10

“Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.”

- Kuna mtu umekuwa ukitenda mema na ni kama vile huoni kama unapata mavuno unayostahili.

- Neno la Mungu linasema, WAAMBIE WATU WENYE HAKI [WATENDAO MEMA], WATAKUWA HERI, KWA MAANA WATAKULA MATUNDA YA MATENDO YAO.

- MATUNDA YA MATENDO YETU NI LAZIMA TUTAYALA, MATENDO YAKO HAYAPOTEI!

- Usikate tamaa katika kufanya mema kwa watu UNAOPATA NAFASI YA KUWATENDEA MEMA, Neno la Mungu linaita huko ni KUPANDA NA LAZIMA UTAVUNA USIPOZIMIA ROHO, YAANI USIPOKATA TAMAA.

- Usikate tamaa katika KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU, usipozimia roho, UTAVUNA 

- Usikate tamaa katika KUISHI MAISHA YA KUMFATUFA MUNGU KWA MAOMBI, KUFUNGA, KUSOMA, KUTOA NK hata kama kwa sasa huoni matokeo unayotarajia; NENO LA MUNGU LIMEKUHAKIKISHIA KWA WAKATI WAKE UTAVUNA.

- NENO la Mungu lililosema kwamba, tutaweka mikono juu ya wagonjwa watapata afya, na tunaona ikitokea, ni hilo hilo lililosema TUTAKULA MATUNDA YA MATENDO YETU, ni hilo hilo linasema TUTAVUNA KWA WAKATI WAKE.

- Neno la Mungu lisingesema TUSICHOKE, kama hakuna hali ya kuchoka kutenda MEMA. Kwa hiyo, hata kama unahisi kuchoka, USICHOKE KATIKA KUTENDA MEMA.

- WAKATI WA KUVUNA LAZIMA UTAFIKA.

Zaburi 126:5-6 “Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha. Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.”

Isaya 3:10 “Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao.”

Luka 18:1 “Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.”

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mw. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!