Uhai wa Imani Katika Yesu Huleta Uzima wa Mwili
Wagalatia 2:20
"....na uhai [life] nilio nao sasa katika mwili [Body, Flesh, meat], ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu”
Neno hilo linalosema "uhai katika mwili" lina maana pia "uzima katika mwili". Na mwili huo ni mwili huu wa nyama.
Paulo anasema, UZIMA ALIONAO KATIKA MWILI, ANAO PIA KATIKA IMANI YA MWANA WA MUNGU (YESU)
Kwa hiyo, KIWANGO CHA UZIMA (UHAI) KATIKA MWILI KINAAMULIWA NA UZIMA (UHAI) KATIKA IMANI YA MWANA WA MUNGU.
Yaani, UZIMA KATIKA MWILI NI MATOKEO YA UZIMA [UHAI] KATIKA IMANI YA MWANA WA MUNGU.
Kwa hiyo kwa kadiri ninavyohakikisha IMANI YANGU INAKUWA HAI katika YESU Kristo, kwa kadiri hiyo hiyo UZIMA WA MWILI WANGU UNAIMARIKA.
KUNA MAGONJWA MENGINE HUTAJUA YALIISHA LINI, MAANA UNAVYOENDELEA KUIMARISHA IMANI YAKO UNAKUJA KUSHTUKA HAUNA TENA HUO UGONJWA.
Imarisha imani yako katika KRISTO YESU, automatically utakuwa unaimarisha afya yako.
Yesu hakuumwa kwa sababu alikuwa na imani timilifu katika Mungu juu ya afya ya Ki-Mungu (Divine Health).
“Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote.” Matendo ya Mitume 3:16 SUV
Andiko hilo nililonukuu linasema wazi kabisa, IMANI KATIKA JINA LA YESU KRISTO, IMANI ILIYO KWA KRISTO, NDIO ILISABABISHA UZIMA MKAMILIFU KWA KIWETE.
KWA HIYO, NI VIZURI KUHAKIKISHA IMANI YAKO KATIKA KRISTO IKO HAI NA UNAILISHA SAWA SAWA... KWA HIYO, ULINZI WAKO UMEHAKIKISHIWA, AFYA KAMILIFU UMEHAKIKISHIWA
“Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.” Yohana 20:31 SUV
na kwa kuamini [kwamba YESU NDIYE KRISTO - IMANI KATIKA KRISTO] mwe na uzima [KATIKA MIILI YENU PIA] kwa jina lake.
Kwa hiyo, unataka kuongeza kiwango cha AFYA/UZIMA KATIKA MWILI WAKO, ONGEZA KIWANGO CHA IMANI YAKO KATIKA KRISTO
Yafuatayo yatakusaidia kuongeza kiwango cha imani yako katika Yesu:-
1) kwa Kusoma Neno lake na Kusikiliza mafundisho ya Neno la Mungu
Warumi 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo”
2) Kulifanyia kazi NENO ulilolisoma au kujifunza,
Yakobo 2:17,26 “Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake ...Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.”
Unapofanyia kazi ulichojifunza unakuwa unaipa mazoezi imani yako...
3) Kwa kuongeza kiwango cha kuwapenda watu
1 Wakorintho 13:2 “…nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.”
Ili imani ikufae, lazima iambatane na upendo kwa watu... Ila imani isiyoambatana na upendo kwa Mungu na watu, inapoteza thamani yake.
Kwa kuwa ninaongelea uzima na afya katika tafakari hii, ni muhimu kufahamu kwamba ukitaka kiwango cha afya yako kiimarike, ni lazima usome sana na ujue sana Neno la Mungu linasema nini kuhusu afya. Ni muhimu sana kutambua HAKI ZAKO ZA UPONYAJI NA AFYA KAMA MWANA WA MUNGU!
Kwa kufanya hivyo, kiwango cha uhai wa imani yako katika Yesu Kriso Mponyaji kitaongezeka na kusababisha kiwango cha afya yako au uzima wako kuimarika pia.
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author