Text

Umeketi Mahali Pa Ulinzi na Afya, Furahia Ulinzi na Afya ya Kiungu

1 views 1 day ago

Zaburi 91:1

Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

Roho Mtakatifu amenipa Neno hili kwa ajili yako ambaye ujumbe huu umekufikia. 

Neno la Mungu linasema katika Isaya 55:11 "ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma."

Neno hili ni kwa ajili ya kutimiza mapenzi ya Mungu kwa kila anayelipokea.

Neno la Mungu linasema MTU AKETIYE au AFANYAYE MAKAO MAHALI PA MUNGU ALIYE JUU, HUYO MTU ATAKAA SALAMA CHINI YA UVULI WAKE MWENYEZI.

Naweka tafsiri ya Kingereza ya Amplified ya andiko hilo hapa chini ili tulielewe vizuri Zaidi.

Psalms 91:1 AMP He who dwells in the shelter of the Most High Will remain secure and rest in the shadow of the Almighty [whose power no enemy can withstand].

Ikiwa na maana "Yeye anayekaa katika makao ya Aliye Juu Atabaki salama na kupumzika katika uvuli wa Mwenyezi (ambaye hakuna adui anayeweza kumuhimili)." 

Kuna mahali panaitwa MAHALI PA SIRI PA MUNGU ALIYE JUU (THE SECRET PLACE OF THE MOST HIGH) ambapo TUKIFANYA HAPO KUWA MAKAO YETU YA KUDUMU, TUTAFUNIKWA NA UVULI WA MWENYEZI MUNGU.

Hapa haongelei maombi ya ulinzi tu bali anaongelea nafasi ya ulinzi. Haiongelei kujiombea ulinzi kwa damu ya Yesu bali anaongelea KUFANYA MAKAO MAHALI PA MUNGU.

Kuna mahali ukikaa, umekaa kwenye usalama, kuna maisha ukichagua umechagua usalama, umechagua kulindwa hata kabla hujaomba.

Mimi ninaamini kila aliyempa Yesu maisha yake na akaelewa kweli hii ya nafasi yake katika Kristo Yesu, hiyo nafasi aliyopo ndio nafasi ya usalama wa hali ya juu sana.

Mara nyingi Shetani hupata nafasi kwa mtu baada ya kupata nafasi kwenye fikra na ufahamu wa mtu kwa kutokujua nafasi yake na haki zake.

Mtu ameokoka lakini mawazo yake yote ni kushambuliwa, ni wachawi, ni kupatwa na magonjwa, ni mauti nk. Ni wazi huyu mtu hajui nafasi yake na huo ndio mwanya Shetani anautumia kutesa watu wengi waliookoka. Fikira zetu haziko sawa sawa na nafasi zetu katika ulimwengu wa roho.

Na Neno la Mungu linasema wazi kwamba, ukiwaza ya wanadamu unakuwa wa shetani.

Marko 8:33 Akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.

Zingatia hapo, hajamwambia unawaza ya Shetani amesema "huyawazi yaliyo ya Mungu, unawaza ya wanadamu."

Ukiwaza ya wanadamu kuhusu AFYA NA ULINZI WA MUNGU, unamruhusu Shetani kuingilia afya yako na ulinzi wa Mungu. 

Kwa LUGHA RAHISI NI KWAMBA, ILI TUFURAHIE NAFASI ZETU, HATURUHUSIWI KUWAZA NJE YA Neno la Mungu.

Kila unachowaza KUHUSU ULINZI NA AFYA ambacho kiko nje au kinyume na Neno hata kama unasema hiki ni cha kibinadamu tu, unafungua mlango wa Shetani kwenye hilo eneo. 

Neno la Mungu linaweka wazi kwamba Sisi tumeketishwa PAMOJA NA KRISTO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.

Waefeso 2:6 Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;

Kwa hiyo, Kila ambacho hakiwezi kumpata KRISTO hakiwezi KUNIPATA NA MIMI kwa sababu TUKO SEHEMU MOJA, mahali pa USALAMA WA MBINGU, KATIKA UVULI WAKE MWENYEZI.Na ukweli ni kwamba HAKIJAKUPATA MPAKA utakapofikiri, kuamini na kukiri kwamba kimekupata. 

Lakini, ili tufurahie nafasi zetu pamoja na Kristo, Neno linatusisitiza katika

Wakolosai 3:1-3 “Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.

Neno linatusisitiza KUTAFUTA YALIYOJUU na KUFIKIRI YALIYO JUU, kama kweli tumeketishwa pamoja na Kristo.

Lazima tugeuze vipaumbele vyetu na kufikiri kwetu (au mawazo yetu).

Kufikiri kwetu ndio mlango (gateway) wa kuishi nafasi zetu tulizonazo rohoni katika ulimwengu wa huu mwili.

Jiulize KWENYE SWALA LA ULINZI NA AFYA, UNAWAZA YALIYO YA MUNGU AU YA WANADAMU? 

Kuna watu linapokuja swala la ULINZI NA AFYA wanawaza TAARIFA ZA HOSPITALI NA MADAKTARI TU, WANAWAZA AKILI ZAO (COMMON SENSE) TU, WANAWAZA MAZINGIRA TU.WATU WA AINA HII HAWATAFURAHIA HAKI YAO KATIKA KRISTO.

Zama hizi tulizoingia sio zama za wataalamu, NI ZAMA ZA KULIAMINI NA KULIISHI NENO LA MUNGU. HEKIMA ZA WANADAMU KUHUSU ULINZI NA AFYA NI MUHIMU LAKINI ZINA UKOMO. USALAMA WETU WA KUDUMU NI KATIKA MUNGU TU.

Ndio maana Neno la Mungu linasema wazi, MWENYE HAKI WANGU ATAISHI KWA IMANI. IMANI KATIKA MUNGU NA ULINZI WA MUNGU NDIO SALAMA YETU ZAMA HIZI. 

LEO UNAWEZA USIELEWE NENO HILI LA BWANA, LAKINI IPO SIKU UTAELEWA. 

Amua kutoka kwenye mawazo na misingi ya kibinadamu kuhusu ULINZI NA AFYA ndipo utaanza kufurahia ULINZI NA AFYA SAWASAWA NA NAFASI YAKO.

Amua kuacha KUTEGEMEA MISINGI YA KIBINADAMU KUHUSU ULINZI NA AFYA, UTAANZA KUONA UKAMILIFU WA ULINZI NA AFYA YA KIUNGU.

Sina ugomvi na hekima na ujuzi wa kibinadamu kuhusu ULINZI NA AFYA, LAKINI NI WAZI KWAMBA VINA UKOMO.

Taarifa sahihi za ULINZI NA AFYA YANGU NI NENO LA MUNGU NA HIZO PEKEE NDIO TAARIFA ZA KWELI.

 Chukua Neno hili, liruhusu lichanganyane na imani ndani yako, utaanza kuona namna linavyokufaa.

Chochote ambacho hujakiamini na kuchukua hatua hakitakuwa na nguvu kwako.

Zaburi 91:1 “Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.”

Mahali ulipoketi ni mahali pa Mungu, ni kwenye uvuli wa Mungu, ni kwenye ulinzi wa Mungu, haparuhusu SHAMBULIO LOLOTE LA KIPEPO WALA LA KICHAWI. NI MAHALI PA ULINZI NA AFYA MASAA 24 NI MAHALI PA UZIMA MKAMILIFU, NI MAHALI PA AFYA KAMILIFU.USIKUBALI WAZO KINYUME NA NENO LA MUNGU.

FIKIRI SAWASAWA NA NAFASI YAKO, WEKA VIPAUMBELE VYAKO SAWASAWA. FURAHIA UZIMA, AFYA NA ULINZI KATIKA UVULI WAKE MWENYEZI. 

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

#Umebarikiwa

~Na Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!