Una Jina la Kuwa Hai Nawe Umekufa
Ufunuo. 3:1b-3
"...Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa. Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu. Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako."
Ninaamini huu ni UJUMBE WA WAKATI NA MUHIMU SANA KWA KILA MKRISTO NA KANISA, SOMA NA UFANYIE KAZI.
Katika maandiko hayo niliyoweka hapo juu, yameanza kwa kusema "Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa"
Ameongelea MATENDO, ameongelea JINA na ameongelea KUFA.
- MATENDO
MATENDO YAKO MBELE ZA WATU YANAONEKANA KAMA UNA UHUSIANO MZURI NA MUNGU
- Anapozungumzia matendo yako, anamaanisha matendo yako ya nje au ya wazi na kazi zako za wazi zinazoonekana na watu wanaokuzunguka.
- Kazi ya Mungu unayofanya, unavyohubiri, unavyoishi kwa nje
- JINA
WATU WANAKUONA UKO HAI NA UNA SIFA NJEMA MBELE ZAO
- Anapozungumzia jina anamaanisha unavyotambulika kwa watu wanaokuzunguka; au sifa zako mbele wa watu.
- Anazungumzia watu wanakuonaje kwa nje?
- Tukitumia Neno la Kingereza, anazungumzia "Reputation: the opinion that people in general have about someone or something, or how much respect or admiration someone receives, based on past or certain perspective.
- Kwa hiyo anapoongelea JINA anamaanisha, mawazo ya kukuhusu wewe, waliyonayo watu wanaokuzunguka, au kiwango cha heshima watu huweka juu yako kutokana na uliyofanya au mtazamo fulani ndani yao kukuhusu.
- KUFA
LAKINI KWA UHALISIA, NDANI YAKO UMEKUFA
- Anaposema umekufa, anamaanisha UHALISIA WA NDANI YA MTU ULIVYO.
- Anaongelea hali halisi ya kiroho aliyonayo mtu ndani yake.
- Haongelei mambo ya nje, haongelei sifa za watu tena anaongelea UHALISIA WA MAISHA YA MTU WA KIROHO ALIVYO.
- Anaongelea SIRI YA MOYO WA MTU.. siri hii ANAIJUA MUHUSIKA, NA YESU PIA ANAIJUA.
- Hapa anaongelea MAISHA HALISI YA MTU, SIO MAISHA YA MAIGIZO, SIO MAISHA YA KUONEKANA NA WATU, SIO MAISHA TUNAYOISHI MADHABAHUNI AU KANISANI.
- Hapa anaongelea MAISHA UNAYOISHI UKIWA PEKE YAKO, hakuna mchungaji wako, wala mtu anayekufahamu...
- Hapa anaongelea maisha yatakayoamua mtu anaenda MBINGUNI au JEHANAMU. SIO YALE YA KUFURAHISHA WATU WANAOTUZUNGUKA TUONEKANE SISI NI WATUMISHI WAZURI WA MUNGU.
YESU ANASEMA HUKU MACHOZI YANAMDONDOKA "Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa."
Japo kuna wakati mawazo yetu na hisia zetu zinatudanganya kwamba Yesu hafuatilii sana details za matendo yetu, lakini ukweli ni kwamba ANAYAJUA SANA MATENDO YETU NA KILA TUNALOLIFANYA.
ANAJUA kabisa kwamba, KWA NJE AU KWA WATU WANAOTUZUNGUKA, TUNAONEKANA TUNAISHI VIZURI SANA... ANAJUA MAJINA YETU YANAONEKANA KUWA HAI.
Yaani tunaonekana TUMEOKOKA, TUNAMPENDA SANA MUNGU, TUNAMTUMIKIA KWA UAMINIFU KABISA YAANI TUNA JINA LA KUWA HAI.
Lakini pia, KWELI INAYOSHITUA NI KWAMBA, ANAJUA KABISA KWAMBA, PAMOJA NA KILA SIFA NJEMA NA MATENDO AU KAZI NJEMA TULIZONAZO NA AMBAZO HIZO HUTUPA HESHIMA KWA WATU, NDANI YETU TUMEKUFA. Na hiyo hali ya kufa kwa ndani ndiyo inayomuumiza.
Anasema, JAPO TUNA JINA LA KUWA HAI, LAKINI NDANI TUMEKUFA.
Haoni UHAI NDANI YA ROHO ZETU.
Uzuri ni kwamba, sio kwamba tu Yesu anajua, bali HATA SISI WENYEWE TUNAJUA KWA HAKIKA UKWELI HUO. Roho zetu zinajua na kutukumbusha turekebishe kila siku.
Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote.
MT. 23:27
- Na bahati mbaya au nzuri ni kwamba, TUMEKUWA MAKINI SANA KUYALINDA MAJINA YETU YASICHAFUKE, kulinda REPUTATION YETU, tukasahau uhalisia wa MAISHA YETU.
Your reputation will not take you to heaven, but pure heart and pure relationship with God will.
Anagalia ushauri anaotoa YESU hapa:
"Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu. Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu."
Nikiweka kwa ufupi ni kwamba, Yesu anashauri TUAMKE, TUANGALIE YALE AMBAYO HAYAJAFA NDANI YETU NA KUKAMILISHA YASIYO KAMILI NDANI YETU.
Ukweli ni kwamba KILA ANAYESOMA UJUMBE HUU ANAJIELEWA NDANI YAKE NI WAPI ANAPASWA KUREKEBISHA. ANAJUA NI YAPI YALIYOSALIA HAYAJAFA YANAPASWA KUIMARISHWA.
Wengi wetu, upendo wetu kwa Mungu haujafa, ndani yetu kabisa bado tunampenda Mungu na tunatamani kuishi maisha ya kumpendeza, na hiyo ni moja ya sababu Mungu ametuvumilia na kutupa nafasi ya kusoma ujumbe huu ambao Roho Mtakatifu anazungumza na kanisa.
Katika Ufunuo 3:3 ndipo hasa anazungumzia namna ya KUFUFUA HALI YA KUFA NDANI YETU.
Anasema: "Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu."
Tafsiri ya Amplified insema:
~‘So remember and take to heart the lessons you have received and heard. Keep and obey them, and repent [change your sinful way of thinking, and demonstrate your repentance with new behavior that proves a conscious decision to turn away from sin]. So then, if you do not wake up, I will come like a thief, and you will not know at what hour I will come to you.
REVELATION 3:3 AMP
Yaani,
1)Kumbuka na uzingatie ndani ya moyo wako, MAFUNDISHO YOTE ULIYOWAHI KUYASIKIA NA KUYAPOKEA.
2) Yatunze hayo, na UTUBU [Uache njia zako na mawazo ya dhambi, na uishi sawa na toba yako, ukiwa na tabia mpya ambayo inadhihirisha maamuzi yako ya kuacha kabisa dhambi.
Wengi tunajua nini cha kufanya ILI KUJIPONYA NAFSI ZETU NA MAUTI HIYO.
Wengi TAYARI ROHO MTAKATIFU ALISHATUKUMBUSHA MARA NYINGI TU KWAMBA TUNAPASWA KUGEUKA.
Kama kuna "Mauti sufuriani", hekima si kuificha bali ni KUPIGA KELELE ZA KUTAKA MSAADA TOKA KWA NABII [MTUMISHI SAHIHI WA MUNGU.]
Kama Shoka limedumbukia majini, hekima si kujikausha, bali ni kusema wapi limedondokea upate msaada.
YESU HAJI NA UJUMBE MPYA, NA YEYE ANASEMA KUMBUKA AMBAVYO AMEKUWA AKIZUNGUMZA NA WEWE, KUMBUKA MAFUNDISHO ULIYOWAHI KUYASIKIA KUHUSU MAISHA UNAYOISHI NA UKISHAYAKUMBUKA HAYO, FANYA MAAMUZI, YAZINGATIE, GEUKA NA UACHE NJIA MBAYA.
Huu ni wakati wa KUWA NA MATENDO NA JINA LILILO HAI, PAMOJA NA KUWA HAI NDANI YA ROHO ZETU PIA.
Anasema USIPOFANYA HIVYO
"Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako."
Ufunuo. 3:22
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
Mwl. Francis Langula
Author