Unafanya Nini Unapokutana na Changamoto/Mabaya? - How Do You Respond To Challenges/Problems?
Yakobo 5:13
“Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.”
James 5:13 (KJVA) “Is any among you afflicted? let him pray. Is any merry? let him sing psalms.”
James 5:13 (AMP) “Is anyone among you afflicted (ill-treated, suffering evil)? He should pray. Is anyone glad at heart? He should sing praise [to God].”
Je ukipatwa na mabaya au Ukitendewa mabaya, au ukiugua ghafla, au ukipata taarifa mbaya ni nini cha kwanza unafanya au unawaza?
- Je Unalia? unamfikiria mama au baba? unamkumbuka uncle? unamkumbuka daktari specialist? Unamkumbuka mkeo au mumeo? unamuwaza mchungaji? unawaza fulani angekuwepo?
- Kama ukipatwa na mabaya unafanya chochote kati ya hivyo au kingine ambacho sijataja, BASI UNAITIKIA VIBAYA, KINYUME NA MAANDIKO, TATIZO LILILOKUPATA [YOU ARE WRONGLY (AGAINST SCRIPTURE) RESPONDING TO THE PROBLEM/CHALLENGE]
- Na kama tunatoa muitikio usio sahihi basi tusitegemee na matokeo sahihi. [If you are wrongly responding to challenges/problems, don't expect correct results.]
- Watu wengi tunaomba tunapokutana na mabaya, lakini TATIZO SIO KUOMBA, TATIZO HATUOMBI WAKATI SAHIHI. WAKATI GANI UNAOMBA BAADA YA KUPATIKANA NA MABAYA INAONYESHA MOYO WAKO UMEMUELEKEA NANI.
- MAOMBI KAZI YAKE MOJAWAPO NI KUMRUHUSU MUNGU KUINGILIA KATI MATATIZO TUNAYOPITIA; KWA HIYO UNAPOOMBA MWISHONI BAADA YA KUJARIBU KILA KITU KIKASHINDIKANA, MAANA YAKE NI KWAMBA, UMERUHUSU KILA KITU AU KILA MTU AINGILIE KATI TATIZO LAKO KWANZA KABLA YA MUNGU NA BAADAYE NDIPO UKAMRUHUSU MUNGU.... KWA HIYO UMEMPA MUNGU NAFASI YA MWISHO; SI AJABU MUNGU AKAZUIA HATA HUO MSAADA TOKA KWA WENGINE/VINGINE.
- Kwa hiyo, ukipatikana na mabaya, ULE MUITIKIO WAKO ni kipimo kizuri sana cha NAFASI YA MUNGU MAISHANI MWAKO.
KUNA WATU TUMEWAWEKA WAJOMBA ZETU (WENYE PESA) KWENYE NAFASI YA MUNGU ndio maana ukipata tatizo tu, unamuwaza uncle wako au mtu fulani, na asipokusaidia UNAMLAUMU NA KUKATA TAMAA...
- Ni kweli Mungu anatumia watu, lakini HAO WATU MUNGU ANAOWATUMIA HAWAPASWI KUCHUKUA NAFASI YA MUNGU YA KWANZA MAISHANI MWETU.
- Mungu yuko tayari kuzuia msaada unaokuelekea kama anayekupa msaada atachukua nafasi ya MUNGU kwenye moyo wako.
Yakobo 5:13 “Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.”
- Sehemu ya pili ya andiko hilo inaonyesha kuwa, kuto-kuomba mara baada ya kukutana na tatizo au changamoto kunaweza kusababisha MOYO WA KUCHANGAMKA KUONDOKA, maana kuna uwezekano mkubwa wa kuwa disappointed na yule mtu ambaye ulidhani angekutatulia changamoto hiyo.
MAOMBI BAADA YA KUPATA MABAYA YATAZALISHA NINI?
Kuna jambo moja la msingi sana LITAFANYIKA UKIMRUHUSU MUNGU KUINGILIA KATI [KUOMBA KWA AJILI YA] TATIZO LILILOKUPATA MARA TU BAADA YA KUPATWA NA TATIZO.
Yakobo 5:13 “Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.”
MAOMBI YATAZALISHA CHANGAMKO LA MOYO NA AMANI
- Hakuna kitu cha muhimu kama kuwa na AMANI NA CHANGAMKO hata kama unapitia CHANGAMOTO;
- AMANI NA CHANGAMKO, vinahifadhi MOYO WAKO USIDHURIKE KWA KILE UNACHOKIPITIA.
- MAGONJWA KAMA VIDONDA VYA TUMBO, PRESSURE, MSONGO WA MAWAZO NA MENGINE MENGI, NI MATOKEO YA KUKOSEKANA KWA CHANGAMKO NA AMANI WAKATI WA CHANGAMOTO ZA MAISHA.
- AMANI NA CHANGAMKO VITAFANYA MAMBO YAFUATAYO MAISHANI MWAKO:-
1. VITAFANYA MACHO YAKO YAWE WAZI KUONA FURSA KATIKATI YA TATIZO,
2. VITAKUFANYA USIWE KIPOFU...
3. VITAKUFANYA UUONE WEMA WA MUNGU KATIKATI YA MAPITO UNAYOPITIA...
4. VITAKUFANYA USIMLAUMU MUNGU...
5. VITAKUFANYA UPIGE HATUA SAHIHI KUELEKEA JIBU LAKO...
Wafilpi 4:6 – 7 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”
- CHANGAMKO NA AMANI ndio hatua ya kwanza ya KUPOKEA MAJIBU YA MAOMBI YAKO. Ndio maana hapo Neno linasema, baada ya kusali, kuomba na kushukuru, Mungu ataachilia AMANI YAKE.
- KWA HIYO AMANI [NA CHANGAMKO] NI KIASHIRIO CHA MAOMBI KUJIBIWA.
- LAKINI PIA AMANI ITAHIFADHI [ITALINDA] MIOYO YETU NA NIA ZETU VISIDHURIKE.
- Lengo la adui kukunyan'ganya hicho kitu chako, au kuleta mashambulizi hayo, kwa kweli lengo lake SIO KUPATA HICHO ALICHOKIHARIBU, bali lengo lake kubwa NI MOYO WAKO NA NIA YAKO. Kwa hiyo, ndio maana Mungu anachofanya anahakikisha UNAPOOMBA, MOYO WAKO NA NIA YAKO VINAHIFADHIWA KIKAMILIFU, WAKATI ANAENDELEA KUJIBU MAOMBI KWA UJUMLA WAKE.
- LENGO LA ADUI NI UHUSIANO WAKO NA MUNGU UVURUGIKE KWA CHANGAMOTO UNAYOPITIA! USIDHANI ADUI ANATAKA HIZO PESA ZILIZOPOTEA, AU ANAFAIDIKA NA HAYO MAGOMVI KWENYE NDOA AU FAMILIA, AU ANAFAIDIKA CHOCHOTE NA MABAYA YANAYOKUPATA; LENGO KUU NI MOYO WAKO NA UHUSIANO WAKO NA MUNGU.
Ayubu 1:11 “Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.”
- Kila jaribu alilopata Ayubu, sio kwamba shetani alikuwa anataka hizo mali zake azitumie, bali alikuwa anautafuta UHUSIANO WA AYUBU NA MUNGU WAKE, ndio maana akasema "naye atakukufuru mbele za uso wako."
- ADUI ANAJUA UMUHIMU WA HUO MOYO WAKO NA NIA YAKO; NDIO MAANA NENO LINASEMA:
Mithali 4:23 “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.”
Mithali 17:22 “Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.”
Yakobo 5:13 “Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.”
KUOMBA NI NJIA YA KUTAFUTA AU KURUHUSU UFALME WA MUNGU KWANZA KWENYE CHANGAMOTO UNAYOPITIA:
>> Neno la Mungu linasema, Mathayo 6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa”
>> Na ufalme wa MUNGU ni Haki, AMANI na FURAHA katika Roho Mtakatifu. Warumi 14:17 “Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.”
>> Na TUMEONA KUWA, MAOMBI HUACHILIA AMANI NA FURAHA
>> Na ukishapata UFALME WA MUNGU - haki, AMANI NA FURAHA [CHANGAMKO] KATIKA ROHO MTAKATIFU; kwa njia ya MAOMBI, NA MENGINE YOTE UTAZIDISHIWA.
UMEPATIKANA NA MABAYA? FANYA JAMBO SAHIHI, MRUHUSU MUNGU AINGILIE CHANGAMOTO YAKO KWA NJIA YA MAOMBI, KABLA YA KUMFIKIRIA MTU YEYOTE; MRUHUSU MUNGU AHIFADHI MOYO WAKO USIHARIBIWE NA CHANGAMOTO ILIYOKUPATA; NA MWISHO KABISA AKULETEE WATU SAHIHI WALIOBEBA MAJIBU YAKO.
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author