Unapokea na Kuamini Taarifa (Report) Gani?
ISAYA 53:1 ”Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa BWANA amefunuliwa nani?”
ISAIAH 53:1 “Who believes our report? To whom is the arm of Adonai revealed?”
Isaya anauliza, ni nani anayeamini taarifa (report) aliyoileta? Kwake huyo MKONO WA BWANA UMEFUNULIWA
Ukisoma sura nzima ya Isaya 53; utagundua TAARIFA hiyo inaonyesha wazi kuwa YESU ALIFANYA YAFUATAYO KWA AJILI YETU:-
Alibeba: MAGONJWA YETU YOTE
Aliteseka kwa ajili ya: MAUMIVU YETU YOTE
Alijeruhiwa kwa ajili ya: UHALIFU WETU WOTE
Alipondwa au alipewa kipondo au alipigwa kwa ajili ya: DHAMBI ZETU ZOTE
Aliadibishwa kwa ajili ya: UZIMA WETU MKAMILIFU
Alichubuliwa vikali kwa ajili ya: UPONYAJI WETU
Kwa hiyo ukiamini TAARIFA hiyo, MKONO WA BWANA u tafunuliwa kwako KUKUTENDEA YOTE YALIYO KWENYE TAARIFA HIYO.
Mkono wa BWANA utafunuliwa na KUBEBA MAGONJWA YETU, MASIKITIKO YETU, HUZUNI ZETU, MAKOSA YETU, MAOVU YETU, MAUMIVU YETU, KUSAMEHE NA KUONDOA UHALIFU WETU, KUSAMEHE NA KUONDOA DHAMBI ZETU, KUSABABISHA UZIMA MKAMILIFU, NA KUPONYA KILA AINA YA UGONJWA!!!
Ukiamini taarifa ambayo sio ya Neno la Mungu, usitegemee MKONO WA BWANA KUFUNULIWA KWAKO.
Tunapoishi du niani, zipo taarifa nyingi mbaya toka kwa madaktari, toka makazini kwetu, toka kwa watu wanaotuzunguka, lakini uamuzi ni wetu kuchagua taarifa ipi tunaichukua na kuiamini!
Taarifa utakayoiamini ndiyo itakayotawala maisha yako... Chagua kuamini TAARIFA YA NENO LA MUNGU MAISHANI MWAKO
NIMEKULETEA TAARIFAYA NENO LA MUNGU LEO, unaweza ukaamua kuichukua na kuiamini.
Uzuri ni kwamba TAARIFA hii ya Neno inaweza kugeuza kila hali uliyonayo, hata kama inaonekana imeshindikana
Isaya 59:1 “Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;”
Ukiamini TAARIFA ya NENO, MKONO WA BWANA HAUSHINDWI KUKUOKOA TOKA KWENYE HUO UGONJWA NA UANGAMIVU!!
JE UNAWEZA KUIAMINI TAARIFA AMBAYO NENO LA MUNGU LINAILETA KWAKO BILA KUJALI DUNIA IMEKULETEA TAARIFA GANI? BASI MKONO WA BWANA UTAFUNULIWA KWAKO KUIGEUZA HALI HIYO INAYOONEKANA KAMA IMESHINDIKANA!
Jifunze kuliamini Neno la Mungu kama lilivyo.
Marko 9:22b-23 “.... lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia. Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.”
Yesu anaweza, na ameshakuhurumia, kinachopungua kwako ni kufanya maamuzi ya kumuamini na taarifa ya Neno lake kuliko kitu kingine chochote!
Ukithubutu kuamini, hata hilo ulilodhani haliwezekani, linawezekana!
Nimechagua kuliamini Neno la Mungu hata kama mazingira yangu yatapiga kelele, hata kama maumivu yakipiga kelele, hata kama maisha yatapiga k elele, NAJUA KWAMBA HILO NENO LA MUNGU LINAWEZA KUGEUZA MAZINGIRA, LINAWEZA KUONDOA MAUMIVU, LINAWEZA KUTULIZA DHORUBA ZA MAISHA.
Fanya maamuzi leo, chagua taarifa ya Neno la Mungu, iamini kama ilivyo na itageuza kila hali.
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula (+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author