Text

Uponyaji na Afya, Mkate Wetu wa Kila Siku (Healing And Health, Our Daily Bread)

1 views 1 day ago

Mathayo. 15:26

Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.

Neno hili Yesu alimjibu yule mwanamke wa mataifa aliyekwenda kumuomba uponyaji kwa ajili ya mtoto wake. 

Wakati Yesu anamjibu huyu mama, mataifa tulikuwa watu wa Mungu lakini hatukuwa watoto wa Mungu, kwa hiyo kisheria wakati wa mataifa kushiriki baraka za Ibrahim ulikuwa bado. 

Kazi nzuri ya Yesu Msalabani ndio ilituhalalisha tukawa na haki kisheria kushiriki baraka za Ibrahim ikiwemo na uponyaji wa Ki-Mungu. 

Yesu alichokifanya msalabani ndicho kilitufanya kuwa WATOTO WA MUNGU. 

Sehemu ya Neno hilo nililonuku     u inasema, "Si vema kukitwaa chakula cha watoto..." 

Sasa kwa maelezo niliyotoa hapo juu tutakubaliana kwamba, anaposema CHAKULA CHA WATOTO anamaanisha UPONYAJI, lakini pia tutakubaliaba kwamba, Kwa zama hizi MATAIFA WANA UHALALI KUSHIRIKI CHAKULA HICHO. 

Kwenye tafakari hii, n     ataka tuangalie zaidi hilo neno CHAKULA CHA WA WATOTO.

Neno hilo chakula cha watoto kwenye tafsiri za asili ni MKATE WA WATOTO (Children's bread), kwa hiyo andiko hilo linasema "Si vyema kuutwaa MKATE WA WATOTO...."

Neno linasema, katika kitabu cha Luka 11:3

"Utupe siku kwa siku riziki yetu." 

Tafsiri ya King James inasema 

"Give us day by day our daily bread." ikiwa na maana, utupatie, siku kwa siku, MKATE WETU WA KILA SIKU. 

Kwa hiyo, KILA SIKU MUNGU ANA MKATE TAYARI KWA AIJILI YETU. 

Tukiunganisha maandiko haya mawili, maana yake ni kwamba, MUNGU ANAO UPONYAJI KWA AJILI YAKO KILA SIKU... LAKINI PIA MUNGU ANAYO AFYA KWA AJILI YETU KILA SIKU... 

Sala hii ya Bwana inaanza kwa kusema, Baba Yetu Uliye Mbinguni.... Maana yake Mungu kama BABA YETU, na sisi ni wanae, ANAO MKATE KWA AJILI YETU KILA SIKU ANAO UZIMA NA AFYA KWA AJILINYETU KILA KUKICHA.

Kama vile alivyo na HEWA NZURI(OXYGEN) KILA TUKIAMKA ANAO NA UZIMA KILANSIKU. 

Kila unapoamka chukua afya yako ambayo Baba ameshakuandalia kwa siku hiyo, kwa hiyo hata ukikutana na vitu vinavyoweza kusababisha magonjwa hayatakupata sababu unao mkate wa siku tayari...

Kama unaumwa, hata leo upo uponyaji kwa ajili yako, unaweza kumuendea Mungu kwa ujasiri kuchukua mkate wako. 

Lakini pia maandiko yanathibitisha kwamba, NENO LA MUNGU NI MKATE, kwa hiyo kila anayesoma Neno la Mungu anakula mkate wa Baba... Kwa hiyo kama ni mgonjwa, MKATE (NENO) UNAYO AFYA NA UPONYAJI  KWA AJILI YAKE. Ndio maana maandiko yanathibitisha kuwa Neno la Mungu ni dawa. 

Jijengee tabia ya KUSOMA NENO NA KULITAFAKARI kila siku, kama ni mgonjwa litakuponya, kama ni mzima litakuongezea kinga. 

Kama NINAKULA MKATE HUU KILA SIKU KWA NJIA YA KUSOMA NENO NA KULITAFAKARI, SIRUHUSIWI KUWA MGONJWA KWA SABABU NINAKULA MKATE WA KILA SIKU AMBAO NI UZIMA WA KILA SIKU. 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)
 

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!