Usihukumu Changamoto Au Ugojwa Kwa Macho Tu, Fanya Hukumu ya Haki
Yohana 7:24
"Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki."
Katika mistari hiyo tunaona ziko hukumu za aina mbili, moja ni Hukumu isiyo haki [hukumu ya macho tu] na mbili ni Hukumu ya haki- Hukumu ya macho imetajwa wazi kuwa ni hukumu isiyo ya haki, lakini hukumu ya haki haikutajwa - KUHUKUMU - Ni kutoa uamuzi wa mwisho juu ya jambo fulani, either kesi au tatizo fulani. Kwa mfano, kitendo cha kusema kwa hali hii anayoumwa, basi hawezi kupona. Hapo maana yake umetoa HUKUMU juu ya hali ya ugonjwa wa mtu.
YESU ameonya TUSIHUKUMU HUKUMU YA MACHO.
HUKUMU YA MACHO ni yale MAAMUZI tunayoyafanya au HITIMISHO tunalolitoa juu ya UGOJWA UNAOUONA KWA MACHO, AU JUU YA TATIZO UNALOLIONA KWA MACHO AU UNALIPITIA.
KILA HUKUMU YA MACHO TU, BIBLIA INAIITA HIYO NI HUKUMU ISIYO HAKI, YAANI SIO HUKUMU YA HAKI.
Hufanyi hukumu ya haki KWA HAYO UNAYOPITIA KAMA UNAFIKIRI MUONEKANO WAKE WA NJE NDIO UTAAMUA HATMA YAKO.
Hiyo hali ngumu ya maisha unayoiona, ukidhani ndio itaamua HATMA YAKO, ujue haufanyi hukumu ya haki.
Neno la Mungu linasema katika 2 Wakorintho 5:7 "Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona."
Kwa hiyo sio sahihi kabisa kufanya maamuzi kwa kutumia MACHO TU [KWA KUONA].
Pia Neno linasema Waebrania 11:6 "Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza;"
Kufanya hukumu kwa macho ni kuenenda kwa kuona, na kuenenda kwa kuona ni kuenenda bila IMANI, na pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa hiyo HAIWEZEKANI KUMPENDEZA MUNGU KAMA UNAFANYA HUKUMU ZAKO KWA MACHO.
HUO UGONJWA UNAOUONA, USIUHUKUMU KWA MACHO, FANYA HUKUMU ILIYOSAHIHI.
NAFANYAJE HUKUMU SAHIHI/YA HAKI?
Yesu alisema namna sahihi ya kufanya hukumu katika Yohana 5:30 "Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka."
Hukumu ya haki ni ile inayofanywa sawa sawa na NENO LA MUNGU
Hukumu ya haki ni inayofanywa sawa na MTU ASIKIAVYO NDANI YAKE [KWA ROHO MTAKATIFU] na sio kama aonavyo nje hali halisi.
Hukumu ya haki ni ile inayofanywa sawa na MAPENZI YA MUNGU [NENO LA MUNGU] JUU YA JAMBO HILO
KAMA UNAPITIA CHANGAMOTO YA UGONJWA AINA YOYOTE, USIHUKUMU SAWA NA TAARIFA YA MADAKTARI, MAANA HIYO SIO HUKUMU SAHIHI, HUKUMU SAHIHI NI SAWA NA NENO LA MUNGU LINAVYOSEMA JUU YA MAGONJWA.
Ni kweli kabisa unasikia au kuona maumivu makali, ni kweli kabisa dunia nzima inasema kuwa ugojwa huo ni wakufisha, ni kweli kabisa, wote waliougua huo ugojwa wamekufa, ni kweli kabisa unasikia au kuona dalili zote za kutokupona, lakini HIYO SIO HUKUMU SAHIHI, HUKUMU SAHIHI NI NENO LA MUNGU JUU YA UGOJWA HUO. HUKUMU SAHIHI NI Zaburi 103:3-4 "AKUSAMEHE MAOVU YAKO YOTE, AKUPONYA MAGOJWA YAKO YOTE, AUKOMBOA UHAI WAKO NA KABURI, AKUTIA TAJI YA FADHILI NA REHEMA" ; HUKUMU SAHIHI NI Zaburi 91:16 "Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu."
Ni kweli kabisa, unaona hali ni ngumu na hakuna mpenyo, ni kweli kabisa kila mtu anaona hivyo, ni kweli kabisa huoni mwisho wala huoni mpenyo, uamuzi au hukumu sahihi sio kukata tamaa;
HUKUMU SAHIHI NI Ayubu. 19:25 "Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi."
HUKUMU SAHIHI NI Warumi. 8:28 "Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake."
KILA UNACHOKIONA KWA MACHO SIO CHA KUDUMU, NDIO MAANA SIO SAHIHI KUFANYA HUKUMU YA MACHO. BALI KILE USICHOKIONA KWA MACHO YA NYAMA[YAANI UNACHOKIONA KWA MACHO YA ROHONI KATIKA NENO LA MUNGU] NDIO CHA KUDUMU; KWA HIYO FANYA HUKUMU KWA KILE UNACHOONA KWA MACHO YA ROHONI KATIKA NENO NA SIO KWA UNACHOONA KWA MACHO YA NYAMA.
2 Wakorintho 4:18 "tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele."
YAANI ILE KWAMBA UMEWEZA KUIONA CHANGAMOTO HIYO AU UGONJWA HUO, HIYO NI UDHIHIRISHO KWAMBA HUO SIO WA KUDUMU; KWA HIYO USIHUKUMU KWA JINSI UNAVYOIONA.
Waebrania 11:3 "Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri."
Yoshua 14:7 "Mimi nilikuwa mtu wa miaka arobaini umri wangu, hapo Musa mtumishi wa BWANA aliponituma niende kutoka Kadesh-barnea ili kuipeleleza hiyo nchi; nami nilimletea habari tena, kama ilivyokuwa ndani ya moyo wangu."
Kilichomtofautisha Kalebu na wale wapelelezi wengine ni hicho, WAPELELEZI WALIHUKUMU KWA WALICHOONA KWA MACHO, KALEBU ALILETA HABARI [ALIHUKUMU] KAMA ILIVYOKUWA NDANI YA MOYO WAKE
USIHUKUMU HUKUMU YA MACHO, USIHUKUMU HUKUMU ISIYOHAKI, HUKUMU KWA HAKI, HUKUMU SAWA NA NENO LA MUNGU, HUKUMU SAWA NA MAPENZI YA MUNGU, HUKUMU SAWA NA ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUSEMESHA NDANI.
KWA HIYO KWENYE KILA CHANGAMOTO, BILA KUJALI UNAONA NINI, TAFUTA KUJUA MAPENZI YA MUNGU [NENO LA MUNGU LINASEMA NINI JUU YA HALI HIYO] KABLA YA KUANZA KUIHUKUMU HALI HIYO.
UKISHAJUA NENO LA MUNGU LINASEMA NINI JUU YA HALI YAKO, INGIA KWENYE MAHAKAMA (KWENYE MAOMBI - UWEPO WA MUNGU) IHUKUMU HALI YAKO SAWA SAWA, NA BAADA YA HAPO ENDELEA KUTAMKA HUKUMU SAWA SAWA NA NENO LA MUNGU!
Kumbuka unahukumu kwa kuona ndani ya moyo wako, kwa maombi yako na matamko (ukiri) yako!
“na furaha yake itakuwa katika kumcha BWANA; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.” Isaya 11:3-4 SUV
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author