Text

Usijisumbue Kwa Neno Lolote

1 views 1 day ago

Wafilipi 4:6-7 SUV

“Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”

“Do not be anxious or worried about anything, but in everything [every circumstance and situation] by prayer and petition with thanksgiving, continue to make your [specific] requests known to God. And the peace of God [that peace which reassures the heart, that peace] which transcends all understanding, [that peace which] stands guard over your hearts and your minds in Christ Jesus [is yours].”PHILIPPIANS 4:6-7 AMP

"USIJISUMBUE", "USIJISUMBUE ", "USIJISUMBUE ".

Kuna mtu au watu tumekuwa tukijisumbua sana na tunayokutana nayo. Yaani unawaza usiku kucha, kiasi cha kukosa usingizi, kiasi cha kuathiri mpaka furaha yako, amani yako na hata maisha yako kwa ujumla.

Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

-- Neno la Mungu linatuambia tusijisumbue kwa neno lolote na badala yake katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru, na tuhakikishe haja zetu zinajulikana na Mungu.

-- Huwezi kusema unaomba na wakati huo huo unajisumbua. Ukifanya kimoja huwezi fanya cha pili kikamilifu. UKIJISUMBUA HUWEZI KUOMBA KIKAMILIFU; na UKIOMBA KIKAMILIFU HUWEZI KUJISUMBUA.

-- Jambo unalojisumbua nalo, au linalokusumbua HUJALIOMBEA KIASI CHA KUTOSHA. UKILIOMBEA KIASI CHA KUTOSHA, HALI YA KUJISUMBUA NDANI YAKO ITAONDOKA.

-- Kujisumbua ni kujaribu kutumia mbinu zako na uwezo wako kutatua changamoto hiyo. KUOMBA, KUSALI NA KUSHUKURU, ni kumruhusu Mungu kuingilia kati hiyo changamoto na kumruhusu akupatie mbinu au mlango sahihi wa kukutoa.

--Ukiona jambo bado linakusumbua, ujue halijajulikana kikamilifu kwa Mungu, yaani hujaliombea kiwango cha kutosha.

-- Kujisumbua kunaliongezea tatizo nguvu machoni pako. Yaani kujisumbua kunaathiri mtazamo wako juu ya changamoto au tatizo.

Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

-- Kiashirio kwamba hujisumbui na jambo hilo, NI AMANI YA AJABU INAYOKUHIFADHI MOYO WAKO NA NIA YAKO

-- Kiashirio kwamba jambo lako au haja yako imejulikana na Mungu, ni pale AMANI ITOKAYO JUU INAPOHIFADHI MOYO WAKO HATA KABLA changamoto haijaondoka.

-- Ukiona bado unahisi usumbufu ndani yako ukiiwaza changamoto hiyo, basi ujue unahitaji kuendelea kuomba mpaka usumbufu uishe na badala yake AMANI IKUHIFADHI MOYO WAKO NA NIA YAKO

-- Na hii ndio sababu YESU alilazimika kukaa kwenye maombi muda mrefu pale mlimani kabla ya mateso. Kila alipokuwa akiacha alikuwa anaona bado moyo wake umebeba HUZUNI kwa kila kilichokuwa mbele yake, lakini baada ya kuomba vya kutosha juu ya hali ile, alipata amani na ndipo akawaambia wanafuzi wake, LALENI SASA.

“Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami. Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe. Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? Kisha akawajia wanafunzi wake, akawaambia, Laleni sasa, mpumzike tazama, saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anatiwa katika mikono ya wenye dhambi.” Mathayo 26:38-40, 45

Unapokutana na changamoto, hitaji la kwanza ni AMANI YA MOYO NA NIA kukabiliana na hiyo changamoto.

-- UKIMRUHUSU MUNGU AINGILIE KATI KWENYE CHANGAMOTO YAKO, JAMBO LA KWANZA ANAFANYA NI KUHIFADHI MOYO WAKO NA NIA YAKO KWA AMANI IPITAYO FAHAMU ZOTE.

KWA NINI AMANI KABLA YA JIBU?

-- Shetani anautafuta MOYO WAKO NA NIA YAKO; Kimsingi, shetani akishambulia AFYA YAKO, HATAFUTI HIYO AFYA YA MWILI bali ANAUTAFUTA MOYO WAKO [KIINI CHA MAISHA YAKO YA KIROHO] NA NIA YAKO[KIINI CHA NAFSI YAKO].

-- Hiyo hasara ya pesa shetani aliyokutia, sio kwamba anachukua hizo pesa azitumie, bali anatafuta MOYO WAKO NA NIA YAKO.

-- Hiyo misukosuko kazini adui aliyoleta, anachotafuta sio hiyo kazi yako maana haimsaidii kitu, bali anachotafuta ni HUO MOYO WAKO NA NIA YAKO.

-- Ndio maana, ijapokuwa MUNGU atashughulika na hiyo changamoto iondoke, lakini kabla ya chochote anahakikisha MOYO WAKO NA NIA YAKO VINAHIFADHIWA SALAMA NA BAADA YA HAPO NDIPO ANASHUGULIKA NA HIYO CHANGAMOTO.

-- AMANI YA MUNGU KUHIFADHI MOYO WAKO NA NIA YAKO ISIPOKUWEPO NDIO UTASIKIA MTU ANASEMA, YAANI BAADA YA CHANGAMOTO ILE NDIO NILIONDOKA NA UGONJWA WA MOYO AU VIDONDA VYA TUMBO.

KWA HIYO NDIO MAANA NENO LA MUNGU LINATUAMBIA "Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru,haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu."

Hakikisha unaomba, unasali na kushukuru mpaka unashawishika HAJA YAKO IMEJULIKANA NA MUNGU. MAANA YAKE NI KWAMBA CHANGAMOTO HIYO HAIKUSUMBUI TENA HATA KABLA HAIJATATULIWA. UKIFIKIA HATUA HIYO, UWE NA UHAKIKA MUNGU ATASHUGHULIKA NA HIYO CHANGAMOTO PIA, NAYO ITAONDOKA.

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!