Text

Usikubali Kutoka Bila Furaha Wala Usipige Hatua Bila Amani

1 views 1 day ago

Isaya. 55:12

"Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya kondeni itapiga makofi."

Kuna mambo kadhaa yamewekwa wazi kabisa kwenye neno hilo. 

Anasema,

#MTATOKA KWA FURAHA

#MTAONGOZWA NA AMANI

#MILIMA NA VILIMA VITATOA NYIMBO

#MITI ITAPIGA MAKOFI

Je unapotaka kutoka eneo moja kwenda lingine unasikia hali gani ndani yako? 

Kabla hujatoka biashara moja kwenda ingine unasikia furaha? 

Kabla hujafanya maamuzi ya kutoka kwenye kuwa peke yako      na kuingia kwenye uhusiano na huyo kijana au binti je unasikia hali gani ndani yako? 

Unapofikiria kutoka kwenda mahali fulani unasikiaje ndani yako?

Je unapoifikiria hiyo biashara unasikia furaha ndani yako? 

Je unapotaka kutoka hiyo kazi kuhamia kwingine unasikiaje ndani? 

Hili Neno linasema, "Maana mtatoka kwa furaha"

Sasa hii si furaha ya nje tu.. Nikimaanisha hii si furaha sababu unajua kuna jambo zuri unakota     ka k     wenda au kile unachotaka kufanya ni kizuri au kina pesa. Hii ni FURAHA YA ROHO MTAKATIFU.

HII NI FURAHA AMBAYO ROHO MTAKATIFU ANAIACHILIA NDANI YA MTU AMBAYO UKIJARIBU KUTAFUTA SABABU UNAWEZA USIIONE. NI FURAHA ILIYOPITILIZA HISIA NA MACHO.

Hii ni furaha ambayo Roho Mtakatifu huitumia ku     tuongoza KUFANYA MAAMUZI YA KUTOKA sehemu moja kwenda nyingine.

Hii ni FURAHA ambayo ROHO MTAKATIFU hutuongoza k     utoka kuelekea MAHALI PENYE MAVUNO MUNGU ALIYOTUANDALIA kama tumekuwa tukipanda na tunasubiri kuvuna. 

Wapandao kwa machozi "Watavuna kwa kelele za furaha. "

ZAB. 126:5

Hii ni furaha ambayo huashiria kwamba tunakota     ka kuelekea NI MAHALI SAHIHI. 

Ukisikiliza furaha hii ndani yako kabla ya kufanya maamuzi yoyote hautakosea maamuzi, siku zote utaamua kuanza jambo kwa usahihi. 

Yaani ukiona ndani yako unakosa furaha au unasikia huzuni maana yake ni kwamba USITOKE au USIFANYE MAAMUZI HAYO hata kama kwa macho ya nje kila kitu kinaonekana kiko sawa. 

Kwa hiyo USITOKE MPAKA UHAKIKISHE FURAHA IKO MAHALI PAKE.  

Kinachofuata BAADA YA KUTOKA NI KUONGOZWA. 

Neno linasema, "Mtaongozwa kwa amani."

Amani itakuongoza katika kupiga hatua sahihi baada ya kufanya maamuzi. 

Kwa mfano, umeamua KUTOKA kuanza biashara fulani, AMANI itakusaidia wakati sahihi, mahali sahihi, watu sahihi wa kuambatana nao nk. 

Au labda FURAHA in     akusaidia KUTOKA kuanza uhusiano fulani kuelekea ndoa, au kwa lengo fulani, AMANI itakusaidia au itawasaidia mtembee njia sahihi katika uhusiano wenu, itawasaidia MSIVUKE MIPAKA kumkosea Mungu, itakusaidia ujue wakati sahihi wa kupiga hatua fulani muhimu. 

Yaani kabla ya kupiga hatua yoyote au kufanya jambo hakikisha UNA AMANI NDANI YAKO. 

KUKOSA AMANI KUNAMAANISHA VITU VIWILI:

Moja, JAMBO UNALOTAKA KULIFANYA AU HATUA UNAYOTAKA KUPIGA SIO SAHIHI

Mbili, INAWEZEKANA NI JAMBO SAHIHI LAKINI SI WAKATI SAHIHI. Si wakati wake. 

Kwa hiyo amani inakuambia subiri kwa muda au acha kabisa.

Ukikubali KUTOKA KWA FURAHA na KUONGOZWA KWA AMANI, Neno la Mungu linasema "Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya kondeni itapiga makofi."

Ni dhahiri kwamba maadamu tunaishi duniani, tutakutana na changamoto mbalimbali, lakini Neno linasem     a Anayetoka kwa FURAHA na KUONGOZWA KWA AMANI, milima na vilima (yaani changamoto) vitatoa nyimbo. 

Yaani changamoto utakazokutana nazo hazitakumaliza bali utaona kitu chema ndani yake. Utaona uhalisia wa Warumi 8:28 "Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake." 

Changamoto unayokutana nayo wakati uko mahali sahihi na njia sahihi kwa sababu ulikubali KUTOKA KWA FURAHA na KUONGOZWA NA AMANI ni tofauti kabisa na changamoto zingine. 

Ndio maana Neno linasema katika ISAYA 43:2 "Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza."

Kuna changamoto unapitia NDANI YAKO UNA AMANI NA FURAHA na huku unaimba wimbo wa ushindi japo nje panaonekana pagumu. 

Usikubali KUTOKA BILA FURAHA YA ROHO MTAKATIFU NDANI YAKO, na usikubali KUPIGA HATUA (hata kama ni ndogo)  BILA AMANI YA ROHO MTAKATIFU NDANI YAKO. 

Kwa sababu Neno Mungu linasema Isaya. 55:12 "Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya kondeni itapiga makofi." 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula

 

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!