Text

Usinitenge na Uso Wako, Roho Mtakatifu Usiniondolee.

1 views 1 day ago

Zaburi 51:11

"Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee."  

Najaribu kuwaza sehemu hii ndogo ya maombi ya Daudi. 

Nagundua Daudi aliona mbali sana... 

Ninaishije mbali na uso wa Mungu(uwepo wa Mungu)? 

Nikiwaza najikuta naomba kama Daudi, "EE MUNGU USINITENGE NA UWEPO WAKO, EE MUNGU USINIONDOLEE ROHO WAKO MTAKATIFU"

Hayo ndio maombi yangu... Ee Mungu, HATA IKITOKEA NIMEKUKOSEA, USINITENGE NA USO WAKO, UWEPO WAKO UNIREJESHE KWAKO... ROHO WAKO MTAKATIFU ANIKUMBUSHE KAMA ALIVYOMKUMBUSHA PETRO ALIPOKUKANA MARA TATU KABLA HUJAENDA MSALABANI. 

Daudi aliona, hakuna janga kama kukaa mbali na uso wa Mungu... 

Moja ya kitu kinaweza kututenga na uso wa Mungu ni DHAMBI... Ni Maisha ya kuizoelea DHAMBI... kuifanya dhambi kuwa rafiki... Ni Kutenda dhambi na kutoishughulikia s     awa na Neno la Mungu linavyosema. 

Isaya 59:2 “lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.

Unapokosea na kuendelea kuizoelea dhambi unasababisha uso wa Mungu ufichwe kwako, na matokeo yake ni HATIA ZISIZOKOMA NDANI YAKO NA MWISHO WAKE NI USHAWISHI WA ADUI KAMA ALIVYOMSHAWISHI YUDA KUJINYONGA... 

Ukikosea na kuamua kwa dhati kuishughulikia DHAMBI SAWA SAWA NA NENO LA MUNGU, MUNGU HAWEZI KUUFICHA USO WAKE KWAKO, BALI ATAZIACHILIA REHEMA ZAKE KAMA ALICHOFANYA KWA PETRO JAPO ALIMKANA YESU MARA TATU. 

Ukifuatilia kabla DAUDI HAJAOMBA MAOMBI HAYA KATIKA MSTARI HUU tulionukuu     u, ALIOMBA MAOMBI MAZITO SANA KUIUNGAMA DHAMBI YAKE... 

Haya yalikuwa ni maombi ya Daudi baada ya Nabii Nathan kumjulisha Daudi dhambi yake ya KULALA NA MKE WA URIA NA KUMUUA URIA. 

Kama utaweza, soma Zaburi 51 kuanzia mstari wa kwanza na k     uendelea... 

Hapa nitaweka mistari kadhaa kabla na baada ya Zab 51:11

Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu iko mbele yangu daima.  Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.   Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya na kuithibiti roho yangu.   Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.   Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya upendo.

Zaburi 51:3, 7-7, 10-12

Kwenye mstari wa 11 Daudi amesema mambo mawili muhimu sana sana... 

Zaburi 51:11 “Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.

Amesema "USO WA MUNGU"... 

Amesema "Roho Mtakatifu"... 

NI BORA KUISHUGHULIKIA DHAMBI KWA GHARAMA YOYOTE ILE KULIKO KUKAA MBALI NA UWEPO MZURI WA MUNGU NA KULIKO KUMKOSA ROHO MTAKATIFU.... 

Ni bora kukubali KUAIBIKA KWA KUTUBU KULIKO KUJARIBU KUFICHA DHAMBI KWA KU     FIKIRI UNATUNZA HESHIMA KUMBE UNAPOTEZA VYA THAMANI.... 

Neno la Mungu linasema, ”Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.“ Ayubu 33:4

Kimsingi, UKIPOTEZA ROHO MTAKATIFU umepoteza UHAI... 

Roho Mtakatifu ndiye anatufanya tuishi, Yeye ndiye anatufanya tuwe na furaha ya wokovu, ndiye anayetuhuisha miili yetu, ndiye anayetuponya, Ndiye anayetupa UHAI... Ndiye MUNGU PAMOJA NASI... Yaani bila yeye HATUWEZI KUISHI... 

NA NDIYE ATATUNYANYUA PARAPANDA ITAKAPOLIA ILI TUNYAKULIWE KUMLAKI YESU MAWINGUNI... 

NDIO MAANA NENO LINASEMA “Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu…” Matendo 17:28a

Binafsi sipati picha MAISHA BILA ROHO MTAKATIFU, MAISHA BILA UWEPO WA MUNGU... 

Ni      Bora kutokuishi kuliko KUISHI BILA MUNGU... 

Ni Bora kufa kuliko kuishi bila Mungu... 

Ndio maana Paulo akasema “Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.” Wafilipi 1:21

Yaani ni FAIDA KUFA UKIWA NA MUNGU, KULIKO KUISHI BILA KRISTO... 

Ndio maana Musa pia akasema “...Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa.“ Kutoka 33:15

"EE MUNGU USINITENGE NA UWEPO WAKO, EE MUNGU USINIONDOLEE ROHO WAKO MTAKATIFU"

Yafanye haya kuwa maombi yako huku ukimaanisha kama Daudi na kuamua kuishi na UWEPO WA MUNGU na ROHO WA MUNGU kwa gharama yoyote ile...  

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula

 

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!