Text

Usiviangalie Vinavyoonekana Maana Vina Mwisho Wake (Expiry Date), Si Vya Kudumu!!

1 views 1 day ago

2 Wakorintho 4:18 SUV

“tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.”

Kila kinachoonekana ni cha Muda tu. Hakuna kinachoonekana ambacho kinadumu milele. KILA KINACHOONEKANA KINA EXPIRY DATE, KINA MWISHO WAKE.

Maadam huo ugonjwa unauona basi sio wa kudumu; Maadam hiyo hali ngumu unaiona maana yake hiyo hali ngumu ni ya muda tu sio ya kudumu.

Shetani amekuwa akigeuza maandiko haya, yaani jambo ukishaliona ndio anakuletea hofu kwamba litakumaliza!

-- Amekuwa anawatisha watu kwamba maadamu ugonjwa huo hospitali wameuona kuwa ni wa kufisha basi utakumaliza!

-- Wakati Neno linasema wazi kabisa, KITENDO CHA KUONEKANA NI KIASHIRIA KWAMBA HILO JAMBO SIO LA KUDUMU!

Naliweka tena hapa andiko letu la tafakari:-

“tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.”

2 Wakorintho 4:18 SUV

Yaani tusiweke macho yetu kwa vinavyoonekana! Yaani, tusifanye maamuzi yetu kutokana na vinavyoonekana! Usijenge msingi kwa vinavyoonekana! 

Usiifikilie hatma yako kwa unayoyaona sasa hivi; usiifikirie hatma yako kwa hali yako ya uchumi unayoiona kwa macho yako sasa hivi; usiifikilie hatma yako kwa kiwango cha elimu ulicho nacho sasa hivi!

Nashindwa nisisitize vipinieleweke, lakini msisitizo uko hapa tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana

Upofanya maamuzi kwa sababu ya unavyoviona kwa macho unakosea sana!

Neno la Mungu linasema MSIHUKUMU HUKUMU YA MACHO BALI HUKUMUNI HUKUMU YA HAKI! Hukumu ya macho sio ya haki; 

“Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki.”

Yohana 7:24 SUV

Kila kinachoonekana kwa MACHO SIO CHA KUDUMU, NI CHA MUDA TU!

KILA KINACHOONEKANA KINA EXPIRY DATE!

Kila hukumu unayoifanya kwa sababu ya unachokiona tu sio hukumu ya haki!

Hiyo hukumu uliyoipatia AFYA YAKO KWA SABABU YA ULICHOONA KWENYE MAJIBU YA DAKTARI HIYO SIO HUKUMU YA HAKI!

Hukumu uliyojipa kwa sababu ya kufeli hiyo mitihani sio hukumu ya haki

Hukumu uliyojipa kwa sababu kuanguka kwa hiyo biashara sio hukumu ya haki

Maadamu hili jambo limeonekana kwa macho basi ujue sio la kudumu!

VISIVYOONEKANA NDIO VYA KUDUMU

“Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele.”

Isaya 40:8 SUV

Kwenye andiko hili nililonukuhu, majani na ua ni vinavyoonekana, kwa hiyo sio vya kudumu, vinanyauka na kukauka; lakini NENO LA MUNGU LINADUMU MILELE!

Kwenye kila unachokiona LIKO NENO LA MUNGU LIDUMULO LINALOWEZA KUNYAUSHA HILO UNALOLIONA!

Ukiona ugonjwa, usiuangalie huo, bali liangalie NENO LA MUNGU JUU YA MAGONJWA LINASEMA NINI

Ukipokea report mbaya usiiangalie hiyo, angalia Neno la Mungu linaloweza kugeuza report mbaya

Kwa hiyo, ambacho kiko kinyume na NENO LA MUNGU kwenye maisha yako HICHO SI CHA KUDUMU! Hakina uwezo wa kudumu milele. 

Kwenye kila kinachoonekana kuna kisichoonekana!

Kwenye UGONJWA UNAOONEKANA KUNA AFYA USIYOIONA 

“mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.”

Warumi 4:17 SUV

ONDOA MACHO YAKO KWA UNACHOKIAONA, ANZA KULIANGALIA NENO LA MUNGU JUU YA HALI HIYO!

Katikati ya bahari ya shamu waliyoiona ilikuwako NJIA WASIYOIONA!

Katika mwamba waliouona Israel kilikuwako kisima cha maji WASICHOKIONA! 

Kwenye lile lile jangwa lililoonekana machoni Hajiri na Ishmael kwamba linawaua; hapo hapo kilikuwepo kisima KISICHOONEKANA kilichowaponya wasife kwa kiu!

Kwenye ziwa lile lile Petro alilokosa samaki usiku kucha, ZILIKUWEPO SAMAKI kwa sababu tu ya NENO LA YESU!

Hiyo hali isiyo ya kudumu unayoiona inahitaji NENO LA KUDUMU ibadilike jumla!

“tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.”

2 Wakorintho 4:18 SUV

Wewe ni shahidi wa maisha yako, ni vitu vingapi ulifikiri vingekumaliza lakini havikudumu wala havikukumaliza!

ACHA KUVIANGALIA VINAVYOONEKANA NA KUKATA TAMAA; LIANGALIE NENO LA MUNGU LINALODUMU MILELE NA LINALOWEZA KUGEUZA KILA SITUATION, LINALOWEZA KUPONYA KILA UGONJWA, LINALOWEZA KUGEUZA KILA CHANGAMOTO!

Mungu hatendi kwa kadiri ya uwezo wako, au kwa kadiri ya elimu yako, au kwa kadiri ya pesa zako au kwa kadiri ya ujuzi wako; MUNGU ANATENDA KWA KADIRI YA UWEZO WAKE NA IMANI ULIYOTAYARI KUIACHILIA KUMUAMINI TU!

IMANI YAKO TU NDIO ITAAMUA MUNGU AKUTENDEE KWA KIASI GANI!

IMANI YAKO NDIO KIFAA AMBACHO KITATUMIKA KULETA UHALISIA WA NENO LA MUNGU MAISHANI MWAKO!

KILA UNACHOKIONA KINAWEZA KUGEUZWA NA NENO LA MUNGU KWA NJIA YA IMANI YAKO KATIKA NENO LA MUNGU!

LIAMINI NENO LA MUNGU KILIKO KITU KINGINE CHOCHOTE, UTAANZA KUONA LIKIGEUZA KILA KINACHOONEKANA KAMA KIGUMU MAISHANI MWAKO!

USIANGALIE VINAVYOONEKANA KWA MACHO YA NYAMA BALI VIANGALIE VINAVYOONEKANA KWA MACHO YA IMANI!

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!