Text

Uvumilivu Ndio Njia ya Ushindi (Endurance Is The Pathway To Victory)

1 views 1 day ago

Mathayo 24:13

“Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.”

Yesu wakati anaongea kuhusu siku za mwisho alisema maneno hayo niliyonukuU hapo juu kwamba, MWENYE KUVUMILIA MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA.

Yaani atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeshinda.

Ndani yangu nimeona tukumbushane kwamba UVUMILIVU NDIO NJIA YA KUELEKEA USHINDI.

Yesu alituhakikishia ushindi lakini hakusema tutapitia njia rahisi kuufikia ushindi.

Hakuna kushinda kama hakuna kuvumilia. Watu wengi tumesahau kweli hii ya Neno la Mungu.

Neno la Mungu linatutaka sana tuwe na UVUMILIVU ili kufikia ushindi. USHINDI tumehakikishiwa lakini NI LAZIMA TUWE WAVUMILIVU.

KUVUMILIA NI KUSUBIRI UNACHOKITARAJIA HUKU UKIFANYA JAMBO SAHIHI UNALOTAKIWA KUFANYA BILA KUACHA WALA KUKATA TAMAA.

UVUMILIVU ni kinyume cha kukata tamaa, MTU ANAYEKATA TAMAA MAANA YAKE AMEKOSA UVUMILIVU.

Viungo (Ingredients) vya mafanikio hav     ijakamilika kama hakuna UVUMILIVU ndani yake.

Ndio maana u     kifuatilia maandiko utaona UVUMILIVU umekuwa msisitizo wa Yesu kabla ya kuondoka duniani.

“Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.” Yohana 16:33

Yesu anasema, najua kabisa kwamba ulimwenguni mnayo dhiki, lakini JIPENI MOYO, MUWE NA UVUMILIVU MTAUSHINDA ULIMWENGU KAMA MIMI NILIVYOUSHINDA.

Sio tu Yesu, hata mitumie pia wamesisitiza sana uvumilivu katika nyaraka mbalimbali.

“ili msiwe wavivu, bali mkawe wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu.” Waebrania 6:12

Ahadi za Mungu zinarithiwa kwa IMANI na UVUMILIVU.

Huwezi kusema una imani kama hauna uvumilivu.

UVUMILIVU sio tu kukubali matokeo bali ni kustahimili hali unayoipitia huku UKIMUAMINI MUNGU KUKUVUSHA, NA KUAMINI SIO KUKAA TU UKISUBIRI BALI NI KUCHUKUA HATUA STAHIKI ILI KUVUKA NA KUSHINDA.

Kama una imani utaendelea kuomba, kufunga na kumtafuta Mungu, na kufanya kila unachotakiwa kufanya mpaka hali hiyo unayoipitia ibadilike au uishinde.

“Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu.” Yakobo 5:10

Manabii wote katika biblia walishinda kwa uvumilivu.

“Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,” Wakolosai 3:12

“mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;” Wakolosai 1:11

“Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini;” Warumi 5:3-4

“Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.” Yakobo 1:4

Hatuwezi kuufikia ukamilifu na utimilifu wa jambo bila kuwa WAVUMILIVU.

“Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,” Waebrania 12:1

LAZIMA TUPIGE MBIO KWA SABURI (UVUMILIVU).

WAKATI UNAPIGA MBIO ZA MAISHA USISAHAU KUWA MVUMILIVU KWA YALE UNAYOKABILIANA NAYO.

Labda nikukumbushe tu, HUWA HATUVUMILII RAHA.

Je unahisi maumivu fulani ya mwili, au maumivu ya nafsi (kama huzuni, kukataliwa, kuumizwa, kutotendewa haki, kusahaulika, kuonewa nk), je unahisi kama kushindwa (failure), unahisi kama una mkosi fulani hivi, unahisi kama kuna upinzani mwingi kuliko wengine, unahisi kama kuna vitu vinakukatisha tamaa nk.

Basi Hapo ndipo UVUMILIVU UNAHITAJIKA.

Tunavumilia KUONEWA, KUKATALIWA, KUAIBISHWA, KUTOTENDEWA HAKI, KUSHINDWA, KUANGUKA, HALI ZA UDHAIFU, KUKOSEWA NA WATU WASIO NA MOYO WA KUOMBA MSAMAHA, KUUDHIWA, KURUDISHIWA MABAYA BADALA YA MEMA, KUTOELEWEKA HISIA ZETU HATA TUKIJARIBU KUJIELEZA, KUELEWEKA VIBAYA MAHALI AMBAPO TULIKUWA NA NIA NJEMA, HUZUNI, HASARA NK.

“tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu - [AMESHINDA].” Waebrania 12:2

Hata Yesu mwenyewe, MUANZILISHI WA IMANI YETU, ili awe mshindi alilazimika KUSTAHIMILI (KUVUMILIA) MSALABA NA KUIDHARAU AIBU.

Kwenye tunda la Roho Mtakatifu, UVUMILIVU NI MOJA WAPO YA TUNDA.

Hakuna mafanikio bila uvumilivu.

Hakuna ushindi bila uvumilivu, UVUMILIVU NDIO NJIA KUELEKEA USHINDI.

Shetani ASIKUDANGANYE KWAMBA WEWE UNA MATESO SANA KULIKO ENGINE, KILA MTU ANAYO MATESO AU CHANGAMOTO HATA KAMA HAIFANANI NA YAKO, NA NJIA YA KUSHINDA KWA KILA MTU NI UVUMILIVU.

Shetani ASIKUDANGANYE kwamba umevumilia vya kutosha inatosha eti ukate tamaa, MWISHO WA UVUMILIVU NI USHINDI, KAMA HUJASHINDA BASI UVUMILIVU HAUJAFIKIA MWISHO ENDELEA KUVUMILIA MPAKA USHINDE.

NA ATAKAYEVUMILIA MPAKA MWISHO TU NDIYE ATAKAYESHINDA.

“Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.” Mathayo 24:13

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!