Text

Wala Hakuna Kitu Kitakachowadhuru

1 views 1 day ago

Luka10:19 SUV

“Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.”

Ukisoma kuanzia mistari miwili kabla ya andiko hili la tafakari utaona kwamba Yesu alikuwa akiwapa Amri hii wanafunzi wake sabini baada ya kuwa wamerudi na kumletea taaarifa ya kazi aliyowatuma!

Kati ya vitu aliwaambia ni, kuhusu amri waliyopewa dhidi ya nguvu za adui shetani, lakini pia ni KINGA DHIDI YA MADHARA AINA YOTE!

-- Amri na Mamlaka tuliyopewa hayaishii tu kwa sisi kutoa pepo, BALI YANA UWEZO WA KUSABABISHA KITU CHOCHOTE CHENYE MADHARA KITAKACHOTUJIA KISITUDHURU.

-- Neno lina sema "wala hakuna kitu kitakachowadhuru", kwa hiyo hapo kwenye KITU, inamaanisha kitu chochote chenye madhara, iwe ni UGONJWA, UCHAWI, MAPEPO, NGUVU ZA GIZA, VIBAKA, MAJAMBAZI, WABAKAJI, SUMU nk vyote haviwezi kutudhuru hata kama ni mashambulizi ya Shetani atakayojaribu kuyatuma eti kwa sababu tumevuruga kazi zake.

-- Biblia ya kingereza inasema kwa kusisitiza zaidi "and nothing shall by any means hurt you" yaani KWA NAMNA YOYOTE ILE, HAKUNA KITU KITAKACHOWADHURU AU WAUMIZA; kwa hiyo, hata shetani ajaribu namna mbali mbali za kutudhuru, HATAWEZA KUTUDHURU.

-- Kwa hiyo hii mamlaka inafanya kazi pande mbili, kwanza ni kumshughulikia adui kwenye maisha yetu na ya watu tunaowahudumia, lakini PILI ni KUHAKIKISHA ULINZI WETU DHIDI YA MASHAMBULIZI YOTE YA ADUI YAWE YA KIMWILI AU YA KIROHO.

Sasa siku zote UHURU NA HAKI YA MTU IMEFUNGWA KWENYE UFAHAMU WAKE! Kwa hiyo hata haki ya ULINZI WA MUNGU KWENYE MAISHA YETU, umefungwa kwenye ufahamu wa mtu kuhusu haki yake ya kulindwa!

Neno la Mungu linasema:-  “tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.” Yohana 8:32 SUV

Kwa hiyo kweli unayoifahamu tu ndio inakuweka huru! Kama hujui kweli ya Mungu kuhusu ulinzi wa Mungu kwako, hautaweza kufurahia ulinzi wa Mungu maishani mwako!

Yesu alisema, WALA HAKUNA KITU KITAKACHOWADHURU!!

Yesu hajachagua baadhi ya vitu, maadamu kina madhara basi hakiwezi kutudhuru!

Tatizo letu ni kwamba kwenye hiyo KITU, tunaweka baadhi ya VITU vyenye madhara lakini vingine tunaviacha!

Tunaamini UCHAWI hauwezi kutudhuru lakini tukikutana na KIBAKA ana bisibisi au silaha, au jambazi tunahisi  hilo jambo YESU hajaliweka kwenye hiyo list ya WALA HAKUNA KITU! 

NENO HILI LINAMAANISHA KILA CHENYE MADHARA HAIWEZI KUTUDHURU, hapo anaposema "HAKUNA KITU" ni kama pameachwa wazi, mimi na wewe ndio tunajaza hicho KITU ni KITU GANI; ukichagua vichache MUNGU ATAKULINDA kwa vichachche; UKIAMUA KILA CHENYE MADHARA, MUNGU ATAKULINDA NA KILA CHENYE MADHARA; ULINZI HUU HAUFANYI KAZI ZAIDI YA UFAHAMU NA IMANI YA MTU; ndio maana Neno linasema "NANYI MNALINDWA NA NGUVU ZA MUNGU KWA NJIA YA IMANI"

“Malaika wa BWANA hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.” Zaburi 34:7 SUV

"Malaika wa Bwana hufanya kituo akituzungukia tunaomcha Mungu na kutuokoa"

ACHA MAISHA YA WOGA NA WASIWASI, TAMBUA HAKI YAKO YA ULINZI NA UANZE KUIISHI!

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!