Yesu Anakuja Upesi, Je, Una Ujasiri wa Kusema Amina na Uje Bwana?
Ufunuo 22:20
“Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu.”
Neno hili NAJA UPESI limetajwa mara kadhaa kwenye Biblia, hasa kitabu cha ufunuo, na kila lilipotajwa kulikuwa na maagizo ya kuwa waangalifu au ahadi fulani iliyoambatana nayo, ISIPOKUWA KWENYE MSITARI HUU NILIONUKU U.
Kwenye andiko hilo nililonukuu, "NAJA UPESI", AMBALO NI TAMKO LA YESU, LIMEFUATIWA NA MUITIKIO wa YOHANA ALIYEANDIKA KITABU HIKI AKISEMA, "AMINA, NA UJE BWANA YESU".
Kuna vitu kadhaa Roho Mtakatifu anatuonyesha kwenye tamko hilo la NAJA UPESI na muitikio huo wa AMINA NA UJE BWANA.
Yesu anaposema NAJA UPESI, kimsingi anazungumzia:-
Moja, kuja kwake KULICHUKUA KANISA LAKE TAKATIFU LISILO NA MAWAA WALA KUNYANZI
“apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na hila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.” Waefeso 5:27
Mbili, anazungumzia MWISHO WA NEEMA YA WOKOVU KWA NJIA YA IMANI.
Yaani ile KUAMINI TU KAZI NZURI YA YESU MSALABANI NA KUIKIRI, HALAFU KUISHI SAWA NA UKIRI BASI UNAKUWA UMEOKOKA, INAKUWA IMEFIKIA MWISHO.
“Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.” Warumi 10:9-10
Lakini, Tatu, anazungumzia MWANZO WA MSIMU MPYA WA AWAMU YA KWANZA YA DHIKI KUU.
Sasa huyu Yohana alikuwa anaelewa haya yote kuhusu kuja kwa Yesu, kwa sababu mengi alifunuliwa Yeye na aliyaandika.
Ule Muitikio wa Yohana, ambao ni kama vile ulikuja automatically, unadhihirisha wazi USALAMA WA MOYO WA YOHANA LINAPOKUJA SWALA LA KURUDI KWA YESU.
YESU ALIPOSEMA TU, NAJA UPESI, PAPO HAPO MOYO WA YOHANA UKAMJIBU NA AKAJIBU AMINA NA UJE BWANA.
Hapa hakukuwa na dakika ya kuanza kufikira nimetenda nini au sijatenda nini. Kabla hujaangalia ulichotenda au usichotenda MOYO MARA NYINGI HUWA UNA MAJIBU SAHIHI WA USALAMA WAKE.
Ukisikia kitu, MOYO WAKO UNASEMA NINI, mara baada ya kusikia, KABLA HUJAKIFIKIRIA SANA HICHO KITU?
Huwa kuna TAARIFA YA MUHIMU SANA INATOKA ROHONI MWA MTU mara tu baada ya kusikia kitu KABLA AKILI HAIJAPATA NAFASI YA KUCHAKATA (KU-REASON).
Sasa tukirudi kwenye andiko letu, HII INAMAANISHA KWAMBA, MOYO WA YOHANA ULIKUWA SALAMA LINAPOKUJA SWALA LA KURUDI KWA YESU NDIO MAANA AKASEMA AMINA NA UJE BWANA.
Je, ukisikia YESU ANASEMA NAJA UPESI, MOYO WAKO UNAKUPA JIBU GANI?
Je moyo wako unasema AMINA, NA UJE BWANA?
Kama, MOYO WAKO UNAJIBU "NAAM NA UJE BWANA", HIYO NI ISHARA YA USALAMA.
Kama, moyo wako hauitikii hivyo, ni ishara kuna kitu kinahitaji kushughulikiwa vizuri ILI KUJA KWA YESU KUSIWE NA HASARA KWAKO. WENGINE MIOYO INAGOMA LAKINI AKILI ZINATUSHAWISHI TUPOTEZEE.
Kuna watu MIOYO YAO INAGOMA KABISA KUITIKIA, HALAFU WANAMTWIKA MUNGU WAJIBU, KWAMBA MUNGU NDIYE ANAYEJUA.
Ukweli ni kwamba, Roho Mtakatifu hushuhudia pamoja na roho zetu kuhusiana na usalama wetu.
Kuna mahali Neno la Mungu linasema, "Mioyo yetu isipotuhukumu, tunao ujasiri..."
Neno la Mungu linasema katika 1 Wakorintho 11:28a "Lakini kila mtu ajihoji mwenyewe..."
Ni hekima ya Ki-Mungu kujihoji mwenyewe KAMA UKO TAYARI KWA UJIO WA YESU AMA LA, KAMA HAUKO TAYARI, NAFASI BADO IPO, BADO HAIJAWA TOO LATE.
NEEMA BADO IPO, JAPO HATUJUI ITAISHA LINI, LAKINI MPAKA SASA BADO IPO.
Ukweli ni kwamba YESU ANAKUJA UPESI, hata kama imeanza kuzungumzwa miaka mingi lakini nyakati hizi tulizonazo IMESHAKUWA KARIBU ZAIDI KULIKO KIPINDI CHA NYUMA.
Kwa hiyo, kila mwenye hekima, HAWEZI KUPUUZIA UKWELI HUO WA YESU KURUDI, NA PIA HAWEZI KUKIFUMBIA MACHO KILE MOYO WAKE UNAJIBU MARA TU BAADA YA KUSIKIA NENO HILO "NAJA UPESI" au "YESU ANARUDI"
Duniani sio kwetu, duniani tunapita, wenyeji wetu ni Mbinguni, tusije tukaishi maisha ya kujisahau kama vile tumefika kumbe tunapita.
Neno la Mungu linasema, Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; "NAJA UPESI"
Je una ujasiri wa kusema "AMINA NA UJE, BWANA YESU"?
Kama una ujasiri sema, AMINA, NA UJE BWANA YESU.
Kama hauna ujasiri huo, HAUJACHELEWA BADO, CHUKUA HATUA SAHIHI KUREKEBISHA NA MUNGU WAKO.
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author