Kanuni ya Kuacha Au Kujikana - Sehemu ya 1
Marko. 10:29-30
Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.
Maneno hayo niliyonuku u, Yesu alikuwa anatoa jibu au maelezo baada ya Petro kusema, "Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe".
Ukifuatilia maelezo hayo ya Yesu utagundua kuna kanuni ya msingi sana ya kuzidishwa au kuongezwa na hiyo ndio nataka tuitazame katika tafakari ya leo.
Yesu alisema, HAKUNA ALIYEACHA, halafu akaanza kutaja orodha ya vitu na watu, kisha akasema maneno mawili ya msingi sana katika kanuni hii ambayo ndio yanatakiwa kuwa dhamira (motive) ya mtu anapoacha hivyo vitu.
1. Kwa ajili ya YESU
2. Kwa ajili ya INJILI
Kisha akasema, matokeo ya KUFUATA KANUNI HIYO, ni KUZIDISHIWA MARA MIA hapa duniani na KUPATA UZIMA WA MILELE MBINGUNI.
Kanuni hii nimeiita KANUNI YA KUACHA, lakini pia naweza kuiita KANUNI YA KUJIKANA.
Je unaweza kuthubutu KUACHA?
Je unaweza kujidhul umu nafsi yako?
Je unaweza kujikana?
Kwa ajili ya Yesu na/au Injili?
Kabla Mungu hajakizidisha kitu kwenye maisha ya mtu, mara nyingi huwa anauangalia moyo wa huyo mtu kwanza umeambatana na hicho kitu kwa kiasi gani. Na njia rahisi ya kujua ni kuangalia kama je unaweza kukiacha au kukitoa hicho kitu?
Kimsingi kushindwa kukiacha au kukitoa kitu (hasa ambacho Mungu anakuhimiza kuacha au kutoa) kwa ajili ya Yesu na/au Injili, ni ishara ya wazi kwamba moyo wako umeambatana na hicho kitu kuliko Mungu, kwa hiyo Mungu hawezi kukizidisha, maana akikizidisha kuna uwezekano kikaukamata moyo wa mtu na kumtoa kwa Mungu.
Kwa hiyo, kila ambacho ninaweza kukiacha au kukitoa kwa ajili ya Yesu na Injili, nimemkabidhi Mungu akizidishe.
Kila ambacho ninaweza kukitoa au kukiacha, ninaweza kukipata mara mia.
Kila ambacho ninaweza kukiacha au kukitoa, sipaswi kupungukiwa na kitu hicho.
Chochote ambacho huwezi kukiacha kwa ajili ya YESU na kwa ajili ya INJILI, umekifanya TASA, umekizuilia ongezeko la KiMungu.
Chochote ambacho ninaweza kukiacha kwa ajili ya YESU na INJILI, nimekipatia UWEZO WA KUONGEZEKA MARA MIA.
- Nikiweza kuacha chakula (kufunga) kwa ajili ya Yesu na INJILI, SITAPUNGUKIWA CHAKULA
- Nikiweza kuacha USINGIZI, kwa ajili ya KUJITOA KWA MUNGU, sitapata tatizo la usingizi maishani mwangu.
- Nikiweza kujizuia PESA YANGU ISINUNUE KITU nikaitumia kwa INJILI, SITAPUNGUKIWA na hicho nilichoacha.
- Nikiweza kutoa Pesa kwa ajili ya Yesu na Injili, Mungu atafungua milango ya kifedha kupitia kazi au biashara au chochote ninachokifanya ili nizidishiwe.
Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji.
MIT. 11:24
- Ili niweze kukizalisha kwa KANUNI HII, lazima niweze kukiacha/kukitoa.
- Ili Mungu atupate sisi, alilazimika kutomzuilia mwanae wa pekee Yesu.
- Ukizuia isivyo haki, umezuia ongezeko.
IBRAHIM alipokuwa tayari KUMUACHA/KUMTOA ISAKA ndipo Mungu alikuwa tayari kutimiza ahadi yake ya kumfanya BABA WA MATAIFA.
Unachokizuilia KWA YESU NA KWA INJILI, Unakizuia kisiongezeke.
- Kama ukiweza kuacha MAHUSIANO ambayo unajua SI SAHIHI, kwa ajili ya Yesu, MUNGU ATAKUPATIA MAHUSIANO SAHIHI.
- Ukiweza kuwaacha watu wasio sahihi kwa ajili ya Yesu, Mungu atakupatia watu sahihi.
Je UNAWEZA KUTHUBUTU KUACHA AU KUTOA KWA AJILI YA YESU NA INJILI? KAMA NDIO BASI MAONGEZEKO NA KUZIDISHWA NI FUNGU LAKO
NITAENDELEA SEHEMU YA PILI YA UJUMBE HUU..
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author