Text

Kanuni ya Kuacha Au Kujikana - Sehemu ya 2

1 views 1 day ago

Marko. 10:29-30 

Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.

MUHIMU: Kama hukufuatilia sehemu ya kwanza, nakushauri fanya hivyo.

Kwenye sehemu hii ya pili ya fundisho hili, nataka nieleze kwa undani kidogo maeneo  mawili aliyosema Yesu.

Maeneo hayo mawili yanajitegemea lakini pia yanategemeana, kama nitakavyoeleza vizuri chini.

1. Kuacha kwa ajili ya Yesu

Hii inazungumzia mahusiano kati ya mtu na Yesu.

Je unaweza KUACHA au KUTOA kitu kwa ajili tu ya kuimarisha au kutoathiri uhusiano wako binafsi na Yesu?

Ili mahusiano ya watu wawili yawe imara, ni lazima kila mmoja awe tayari KUACHA au/na KUTOA vitu fulani kwa AJILI YA MWENZIE.

Kama tunataka uhusiano wetu binafsi na Yesu uwe imara, ni lazima tukubali kujikana na kuacha vitu fulani na kutoa kwa ajili tu YA YESU.

Ni lazima tukubali KUACHA TABIA FULANI KWA AJILI TU YA YESU, TUACHE MAHUSIANO NA WATU FULANI (HATA KAMA YANAONEKANA YANA FAIDA KWETU), YANAYOTUSABABISHA TUSIHUSIANE VIZURI NA YESU, KWA AJILI YA YESU.

Ni lazima tukubali KUTOA MUDA WETU KWA AJILI YA YESU ILI KUIMARISHA UHUSIANO WETU NA YESU. Tutoe muda wa kusoma Neno, kuomba, kuutafuta uso wa Mungu (hata kama hatujisikii), kwa ajili tu ya uhusiano wetu na Yesu.

Ni lazima tukubali kuacha vitu vinavyotufurahisha kwa ajili ya kuimarisha uhusiano wetu na Yesu.

Lazima tukubali wakati mwingine KUACHA USINGIZI, STAREHE, TV, SIMU nk      kwa ajili ya kufanya vitu (kuomba, kusoma neno, kutafakari nk) ambavyo vitaimarisha uhusiano wetu na Yesu.

Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha.

MK. 8:35

Ni lazima tukubali kuzidhul     umu nafsi KWA AJILI YA YESU.

Ili mahusiano yoyote yawe imara, ni lazima wanaohusiana wakubali kulipa gharama. Mahusiano huhusisha UPENDO(LOVE), NA UPENDO SIKU ZOTE NI GHARAMA (LOVE IS ALWAYS EXPENSIVE)

- Ndio maana ilimlazimu Mungu kulipa gharama ya kumtoa mwanae ili kuhusiana na sisi.

- Na sisi tunayo gharama ya kulipa kuhakikisha UHUSIANO HUU      UNAIMARIKA.

-Gharama ni KUACHA/KUTOA kwa ajili      ya Kristo.

- Ukiangalia kwa kweli MWILI WAKO NA NAFSI YAKO vingependa hicho kitu, lakini KWA AJILI YA YESU TU, UNAAMUA KUKIACHA AU KUKITOA.

- UNAIDHUL     UMU NAFSI YAKO NA MWILI WAKO KWA AJILI YA YESU.

- Je unaweza kuyaangalia maisha yako wewe binafsi kwa undani? Je ukijipima haugundui kuna vitu vingi sana vinaathiri UHUSIANO WAKO NA YESU (Vinakuzuia usihusiane naye vizuri) ? UNAWEZA KUAMUA KUANDIKA ORODHA (LIST)  YA HIVYO VITU NA KUFANYA MAAMUZI YA KUVIACHA KWA AJILI TU YA YESU hata kama NAFSI YAKO NA MWILI WAKO UNAVUTWA KWAVYO?

Orodha hiyo ya vitu vinavyoathiri uhusiano wako na Yesu inaweza kuwa na vitu kama:-

▪Dhambi inayokuzinga upesi (inayojirudia rudia) na maisha ya dhambi kwa ujumla

▪Marafiki wasiofaa na mikusanyiko isiyofaa (bad      company)

▪Mahusiano yasiyo sahihi (yanayomkosea Mungu)

▪Matumizi mabaya ya muda (muda kwenye vipindi vya TV, Movies, Entertainments nk)

▪Mazungumzo mabaya

Orodha hii inaweza kuendelea zaidi, nimeweka tu kama mfano.

- Lakini pia, JE, UNAWEZA KUANDIKA LIST YA VITU AMBAVYO UMEKUWA HUVIFANYI KWA UAMINIFU JAPO UNAJUA WAZI UKIVIFANYA VITAIMARISHA UHUSIANO WAKO NA YESU?  NA UKISHAVIANDIKA UNAWEZA UKAAMUA KWA DHATI KUANZA KUVIFANYA KWA UAMINIFU KWA AJILI YA YESU TU?

Orodha yako itakuwa na vitu kama:-

▪Maisha endelevu ya maombi

▪Maisha endelevu ya kufunga

▪Maisha endelevu ya kusoma na kutafakari Neno la Mungu

▪Maisha endelevu ya kusoma vitabu vya mafundisho

▪Maisha endelevu ya k     usikiliza mafundisho ya Neno la Mungu

▪Maisha endelevu ya Ibada

Na vingine vingi

TUKIFANYA HIVYO, NDIPO TUNAWEZA KUPATA KWA UKAMILIFU FAIDA ZA KUWA NA UHUSIANO NA YESU AU KUOKOKA.

Mungu alipomuachilia Yesu kwa ajili yetu, hakuna ambacho alizuilia... Alimuachilia na kila kitu tunachohitaji.

Alimuachilia na Nyumba, mali, watoto, watu sahihi, utajiri, heshima nk, tutakapofanikiwa eneo hili la UHUSIANO MZURI NA YESU, hakuna kitakachotuzuilia mara mia ya kila tutakachokiacha... Lakini pia PAMOJA NA UZUMA WA MILELE.

Inawezekana kupata hivyo na wakati huna uhusiano mzuri na Yesu, lakini ITAMFAIDIA MTU NINI KUPATA ULIMWENGU WOTE NA KUPATA HASARA YA NAFSI YAKE JEHANAM MILELE? Ni BORA KUWA NA UHUSIANO MZURI NA YESU, NA VYOTE UPATE KAMA BARAKA TOKA KWAKE.

2. KWA AJILI YA INJILI

Eneo la pili ambalo napenda kulizungumzia ni KUACHA KWA AJILI YA INJILI.

Eneo hili hasa ninaweza kusema KUTOA KWA AJILI YA INJILI.

Hili ni eneo Muhimu sana sana, na ndio maana Yesu alilizungumzia hapa kwenye KANUNI YA KUACHA.

Kila mtu aliyeokoka, NINLAZIMA AFANYE KITU KWA AJILI INJILI.

INJILI ni habari njema ya Yesu (Neno la Mungu)      inazogeuza maisha ya watu.

Kila Mkristo ana wajibu wa kupeleka injili, yaani kuwaambia WATU HABARI ZA YESU. LAKINI PIA ANA WAJIBU WA KUTOA PESA NA NGUVU ZAKE KWA AJILI YA      KUHAKIKISHA INJILI INAENDA.

Hapa kuna      vitu vitatu muhimu, moja ni wajibu wa kila mtu aliyeokoka kuhakikisha anawaambia watu wanaomzunguka habari za Yesu, na katika kufanya hivyo ni lazima KUJIKANA. Jambo la Pili ni kwa wale ambao WANA WITO WA KUFUNDISHA/KUHUBIRI NENO/INJILI KWA MUDA WOTE (FULL TIME MINISTERS) wakubali kuacha vitu ambavyo kwa watu wengine ni ngumu kuacha, KWA AJILI YA INJILI. Na Jambo la Tatu, ni KUKUBALI KUTOA KWA AJILI YA KUSHIRIKIANA NA WALE WALIOJITOA MUDA WOTE ILI WAPELEKE INJILI.

Kutoa KWA AJILI YA INJILI NI JUKUMU LA KILA MTU ALIYEOKOKA.

Ni vizuri kujipima kama wewe moyo wako uko kwa injili kiwango gani. Na njia moja wapo ya kujiangalia ni kuangalia asilimia ngapi ya mapato yako inatumika ku support injili au kuujenga ufalme wa Mungu.    

Mungu akigundua kipaumbele chako katika mapato yako ni UFALME WA MUNGU, hawezi kukuzuilia KUZIDISHIWA.

Kila tunachokifanya, kipaumbele chetu kinatakiwa kuwa ufalme wa Mungu.

Ukweli ni kwamba, kila aliyeokoka anapaswa kuhakikisha ufalme wa Mungu/injili ndio unakuwa kitu cha kwanza kwake na ndipo tutaona mengine yakizidishwa.

Bali utafuteni KWANZA ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Mathayo 6:33

Kingdom minded people are qualified for God's blessings.

Kila anachotupatia Mungu, kusudi lake namba moja ni kuujenga ufalme wa Mungu...

Haya maeneo mawili HUFANYA kazi kwa pamoja, NI LAZIMA TUACHE/TUJIKANE/TUJITOE KWA AJILI YA UHUSIANO WETU NA YESU lakini pia TUTOE/TUJITOE KWA AJILI YA INJILI.

Tukifanya hivyo maana yake tunafuzu kuzidishiwa mara mia sasa na baadaye Uzima wa Milele.

Uhusiano mzuri na Yesu unatuhakikishia Uzima wa milele, kuipeleka injili na kuutanguliza ufalme wa Mungu kunatuhakikishia mara mia katika ulimwengu huu...

Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.

MK. 10:29-30 SUV

Je UNAWEZA KUTHUBUTU KUACHA/KUJIKANA/KUTOA/KUJITOA KWA AJILI YA YESU NA KWA AJILI YA INJILI? KAMA NDIO, BASI KUZIDISHIWA NI LAZIMA.

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)
 

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!