Text

Mwanangu Nipe Moyo Wako - Sehemu ya 1

1 views 1 day ago

Mithali 23:26

“Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu.”

Mungu anautaka moyo wako na wangu. 

Ninaamini huu ni wito kwa kila mtu, ni sauti ya Mungu kwa watoto wake. 

Mungu anasema, "Mwanangu nipe moyo wako"

Watu wengi tunasema tunampenda Mungu na kumuabudu kwa mioyo yetu yote lakini si kweli.

Watu wengi mioyo yetu tumewapa watu na wengi pia tumeikabidhi mioyo yetu kwa vitu mbali     mbali. 

Wengine wamewapa mioyo yao      wapenzi wao, waume wao au wake zao, wengine mioyo yao wameikabidhi kwa watoto wao, wengine kwa pesa na mali walizonazo... 

Mungu anautaka moyo wako. 

WAJIBU WA K     UMPATIA MUNGU MOYO WAKO NI WA KWAKO NA SI WA MUNGU

Mungu anataka AKA     BIDHIWE KWANZA MOYO ndipo aumiliki na kuusaidia. Usipomkabidhi hatafanya chochote. 

Kuna vitu vingi vinaweza kujulisha kama moyo haujakabidhiwa vizuri kwa Mungu... 

Kimojawapo ni jinsi gani moyo wa mtu HUMTUMAINI MUNGU... 

Kama kweli UMEMKABIDHI MUNGU MOYO WAKO 100%, UTAMTUMAINI 100%.

Sasa bila kuelezea kwa kina, watu wengi tunaweza kujibu kirahisi tu kwamba "MIOYO YETU INAMTUMAINI MUNGU"

Leo nataka niongelee eneo moja tu la kujicheki moyo wako kama kweli unamtumaini Mungu. 

Neno la Mungu linasema

"Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;" 

Mithali 3:5

Akili zinatumiwa hazitegemewi... 

Unajuaje unamtumaini Bwana Kwa Moyo wako Wote? 

Unajuaje hautumainii vitu? 

Unajuaje hautumai     nii mali zako? 

Unajuaje hautumainii kazi yako? 

Unajuaje hautumainii watu? 

Majibu ni rahisi, jaribu kujiuliza ikitokea umepoteza hiyo kazi au hizo pesa zote ghafla, nini kitatokea kwa moyo wako? Au ikitokea uhusiano na huyo mtu unevunjika ghafla? 

Je ukiwaza hivyo unasikia kama moyo kupasuka?  Unaona kama vile huwezi kuishi tena bila hivyo vitu au bila huyo mtu? Hiyo ni ishara kwamba moyo wako unatumainia zaidi hivyo vitu au mtu kuliko Mungu. 

Moyo unaomtumaini Mungu unawe     za kuendelea kuwa salama katika hali zote.... 

Swali lingine, je ukipata changamoto au tatizo la ghafla, ni nani au ni kitu gani huja moyoni mwako kwanza? 

Je unawaza mshahara wako kwanza? Je unamuwaza mtu fulani kwanza? Au kitu fulani ulichonacho kwanza?

Kama ndivyo, Hiyo ni ishara, moyo wako umeviweka hivyo vitu au hao watu kwanza na bila wewe kujua, unavitumainia kuliko Mungu... ANAYEKUJIA MOYONI Kwanza baada ya Changamoto, ndio moyo wako umemuelekea yeye... Hata kama ni mume au mke, hata kama ni baba au mama au mtu wa karibu, bado hapaswi kuchukua nafasi ya kwanza ya Mungu kwenye moyo wako. 

Lakini pia, Chochote ambacho kinaweza kuufanya moyo wako kukiwaza hicho kiasi ambacho ukaacha au ukashindwa kufanya mambo ya Mungu, ujue hicho kitu kwa namna moja ama nyingine moyo wako umekitumaini. 

Kama kukosa pesa au kupungukiwa kunaweza kukufanya ukapunguza ibada na mambo ya Mungu kama maombi, kufunga kusoma Neno nk, maana yake moyo wako unatumainia pesa kuliko kumtumaini Mungu. 

Kama ukipata pesa na mafanikio unajihisi moyo wako unakosa ladha ya mambo ya Mungu, ni ishara kuwa moyo wako unazitum     ainia pesa na mafanikio kuliko Mungu. 

Nimejaribu kuweka maswali machache na m     ifano michache lakini ni muhimu sana kuifahamu mioyo yetu... 

Mungu anasema, 

Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu.

Mithali 23:26 SUV

Mungu anatusisitiza tumpe mioyo yetu... 

Neno la Mungu linasema, 

Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?  Yeremia 17:9

Usip     ompatia Mungu moyo wako, ni rahisi sana moyo kukudanganya... 

Kwamba bila huyu wewe huwezi kuishi, NA KUMSAHAU MUNGU ALIYEMUUMBA HUYO na wote.... 

Bila kazi fulani wewe utakufa masikini au hutafanikiwa, na kumsahau MUNGU ALIYEKUPA HIYO KAZI.. 

Sio tu kudanganya, moyo unaweza hata kumpeleka mtu kwa mauti... 

Moyo usiokabidhiwa kwa MUNGU, UNA UGONJWA WA KUUA... 

SALAMA YA MOYO WAKO SI KUMPA RAFIKI YAKO UNAYEMUAMINI, SI HATA KUMPATIA MUME WAKO AU MKE WAKO, SIO HATA KUUKABIDHI KWA FEDHA NA MALI... 

SALAMA YA MOYO WAKO NI KUMPATIA MUNGU, YEYE AWE NAFASI YA KWANZA, VINGINE VYOOOTE VIFUATIE. 

IFIKE MAHALI KUKOSA KITU, CHANGAMOTO, MAJARIBU, KUFANIKIWA NK, VYOTE HAVIHARIBU MAHUSIANO YA MOYO WAKO NA MUNGU... 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula

 

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!