Text

Mwanangu Nipe Moyo Wako - Sehemu ya 2

1 views 1 day ago

Mithali 23:26

Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu.

Mahali salama pa kupeana mioyo yetu ni kwa Mungu, Baba yetu.

The safest place TO GIVE FULLY YOUR HEART IS TO GOD, OUR FATHER.

Mungu hata ku disappoint, he is always available for you, when you need Him at midnight He is available, He never sleeps nor slumber... His help is always available.

Ukimuhitaji usiku wa manane anapatikana, yeye halali wa hasinzii... Msaada wake siku zote upo.

Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.

ZAB. 121:4

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

ZAB. 46:1

He is never too busy to respond, He is never too occupied to ignore you.

Hakuna siku ana kazi nyingi kiasi cha kushindwa kukuitikia, hakuna siku amekamatika kiasi cha kukupuuzia.

He is always a caring Father, Ni baba anayejali siku zote.

He is all powerful. Anazo nguvu zote tunazohitaji.

There's nothing too big to Him, nothing too hard to Him.

Hakuna jambo gumu wala kubwa la kumshinda.

He's not moody, He is never out of mood.

Haendeshwi  na hisia bali yeye ni mwaminifu kwa Neno lake.

Hakuna siku hajisikii kuongea, hakuna siku hajisikii kukusikiliza, hakuna siku ameishiwa na msaada.

He's always welcoming, He is ALWAYS CALLING YOU.

Siku zote anatukaribisha kwake, siku zote anatuita kwake.

Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Mathayo 11:28

Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila gharama.

Isaya 55:1

Although He's the most expensive and valuable Father but He never charge for consultation fee becaused He knows no one can afford so He decided to come to us FOR FREE THROUGH JESUS.

Ingawa ndiye BABA wa thamani na gharama kuliko wote, lakini hatulipishi chochote kumuendea kwa sababu anajua hatuwezi kumudu hiyo gharama kwa hiyo akaamua kuja kwetu bure kupitia Yesu.

Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu.

Ukifuatilia maneno hayo,  mistari kadhaa juu na mistari kadhaa chini, utagundua USIPOMPA MOYO WAKO BABA (MUNGU) YAKO KIKAMILIFU, basi moyo wako utapata shida kuhusiana na watu.

Anaposema nipe moyo wako anazungumzia MAHUSIANO.

Japo wengi hatufahamu, LAKINI WANADAMU TUNAHUSIANA KWA MIOYO pia.

Sisi kwa sisi tunahusiana kwa mioyo yetu, LAKINI PIA TUNAHUSIANA NA MUNGU KWA MIOYO YETU.

Mahusiano yoyote ya watu wawili huhusisha mwili na moyo (ikiwa na maana ya nafsi na roho ya mwanadamu).

Hii inat     hibitishwa na mfano wa Lazaro yule masikini na Tajiri.

Wakiwa duniani, walihusiana kwa miili, lakini kwa sababu mioyo (nafsi na roho) yao ilihusiana pia ndio maana hata baada ya kufa (kuwa nje ya mwili) bado waliweza kufahamiana na hata kuhusiana kwa namna fulani.

Ili tuweze kuhusiana na watu kwa usalama, NI LAZIMA TUHUSIANE KWANZA VIZURI NA MUNGU KAMA BABA.

Ukihusiana vizuri na Mungu Baba, atakusaidia namna sahihi ya kuhusiana na watu.

Moja ya kazi alikuja kufanya Yesu ni Kuganga mioyo iliyovunjika, na mara nyingi sana MIOYO HUJERUHIWA NA WATU TUNAOHUSIANA NAO, kwa hiyo ILI YESU AUGANGE NDIO MAANA ANATAKA TUMPATIE YEYE KWANZA, TUHUSIANE VIZURI NA YEYE KWANZA.

Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; AMENITUMA ILI KUWAGANGA WALIOVUNJIKA MOYO, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.

ISA. 61:1

Mtu mwepesi kujeruhiwa moyo au aliyejeruhika moyo sana NI ISHARA YA WAZI KWAMBA ANA TATIZO KATIKA KUHUSIANA KWAKE NA BABA YAKE, HAJAMKABIDHI KIKAMILIFU MOYO BABA (MUNGU) YAKE.

Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu.

MIT. 23:26

Andiko hili linasema MWANANGU, halisemi      MTU WANGU au KIUMBE CHANGU.

Linapokuja swala la mahusiano kwa mioyo yetu, hatuendi kwa Mungu kama muumbaji wetu au kama watu wa Mungu, bali TUNAMUENDELEA KAMA BABA.

Mungu hawezi kuhusiana na miti, wanyama, ndege nk kwa sababu hivyo vitu yeye  ni MUUMBAJI wake na sio Baba kwao.

Linapokuja swala la MAHUSIANO, SIO TU NI MUNGU WETU au NI MUUMBA WETU, BALI NI BABA YETU.

Linapokuja swala la KUMPA MUNGU MOYO, NI LAZIMA UHUSIANE NAYE KAMA BABA NA SIO KAMA MUUMBAJI TU.

Mahusiano ya Baba na Mwana yana uzito mkubwa sana.

- Yanamaanisha umoja (oneness) - cha Baba changu, na changu ni cha Baba.

Mimi na Baba tu umoja.

YN. 10:30

Huzuni zangu zote nambebesha, furaha yake yote naichukua...

MAJERAHA yote ya moyo namshirikisha, AMANI YAKE YOTE NINAISHIRIKI.

- Yanamaanisha Moyo (wa Baba)  kwa moyo (wa mtoto).

Siri za Moyo wangu zote ninamueleza, na Roho wake Mtakatifu ananifunulia siri za Baba yangu.

Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.

1 KOR. 2:10-12

- Yanamaanisha kila cha Baba ni chetu.

Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake.

YN. 3:35

Kwa ufupi, Mungu anapotaka tumpatie mioyo yetu, ana mambo mazuri sana kwa ajili yetu yatakayoambatana na uhusiano huo.

Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu.

Ukimpa Mungu moyo wako, utahusiana vizuri na yeye. MAHUSIANO YENU NDIO YATAKUWA KIPAUMBELE.

Yaani, jambo lolote ambalo LITAATHIRI UHUSIANO WA MOYO WAKO NA MUNGU, UTAKUWA TAYARI KULIACHA KWA GHARAMA YOYOTE.

UTAPENDEZWA NA NJIA ZA MUNGU TU, PASIPO NA NJIA ZA BABA YAKO HUWEZI KUPAFURAHIA.

MAHALI SAHIHI NA PA USALAMA PAKUPELEKA MIOYO YETU, NI KWA MUNGU, BABA YETU.

TUKITAKA SALAMA YA KUHUSIANA NA WATU LAZIMA TUHUSIANE KWANZA VIZURI NA MUNGU BABA YETU, NI LAZIMA TUMPE MUNGU MIOYO YETU

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula

 

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!